Taekwondo waja na semina kwa wanawake

0
985

Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam

Uongozi wa Chama cha Taekwondo Mkoa wa Dar es Salaam (DTA) umesema umeandaa semina Maalum kwa wanawake ambayo imepangwa kufanyika baadaye.

Akizungumza kwenye semina ya wakufunzi wa mchezo huo iliyofanyika Januari 22, mwaka huu, Mkurugenzi wa Ufundi wa DTA Majaliwa Patrick, amesema walengwa wale wa semina hiyo ni Wanawake wasioufahamu mchezo huo .

Patrick amesema lengo ni kuwafundisha kwa kuwaelezea faida zake, ushiriki katika mashindano mbalimbali ili kuwaondoa katika mtazamo hasi kwa wanawake.

Amesema kuwa washiriki hao watatoka vyuoni, shule mbalimbali kwa nia ya kuhamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchezo huo.

“Kwa sasa ni changamoto ya kitaifa kwa Wanawake kujitokeza katika ushiriki mbalimbali,lakini sisi tumekuwa tukitoa ofa kwani tunahitaji wawe wanashiriki kikamilifu na jitihada zinaendelea kufanyika,” amesema Patrick.

Naye, Katibu Mkuu wa DTA, Erasto Golyama, amewataka wakufunzi hao wanatakiwa kwenda kufanya kwa vitendo yale waloojifunza katika maeneo yao.

Amesema watakuwa na jukumu la kuwaandaa wanafunzi, wachezaji mbalimbali kutoka kwenye vilabu.

“Tunaamini tutakwenda kuifanyia kazi elimu tuliyoipata na tutakuwa tukifundisha kwa mfumo mmoja na kubadili utaratibu wa kila mmoja kufundisha kwa njia tofauti,” amesema Golyama.

Wakufunzi 23 wamefaidika na semina hiyo ambayo ilifanyika kwa siku moja jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here