Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Peter(TAEC) imesema kuwa teknolojia ya mtambo maalum wa kuhifadhi mazao itasaidia kuhifadhi vyakula na mazaao hatua itakayoonggeza muda wa matumizi ikiwamo kuzikinga dhidi ya uharibifu unaoweza kuleta vimelea na vya vijidudu.
Akizungumza Katika Maonyesho ya 45 ya Kimataifa ya Bishara ya Sabasaba yanaoendelea jijini Dar es Salaam, Vitus Abel ambaye ni Mtafiti amesema kuwa tayari tume hiyo ipo katika mchakato wa kuanza ujenzi wa mtambo huo maalum lengo likiwa ni kuziongezea muda wa matumizi bidhaa za mazao nchini.
Abel teknolojia ya nyuklia inayojumuisha mionzi ya gamma, Xrei na elektroni (e-beam) hunurisha bidhaa mbalimbali za mazao ya kilimo, viwandani na vifaa vya matibabu ili kuua vijudu viharibidu na kuimarisha ubora wa bidhaa.
“Niseme tu kwamba teknolojia hii ina faida kubwa katika kuboresha huduma za afya, chakula, mazao na kuboresha mazingira hivyo kuchangia ukuzaji uchumi wa nchi.Teknolojia hii pia itaweza pia kutumika kwenye bidhaa za usafi, matibabu, waya, semiconductors, vifaa vya polymeric na uponyaji / makovu ya nyuso, phytosanitary na kupunguza uchafuzi wa mazingira,”amesema Abel.
Abel ameongeza kuwa kwa sasa bado Tanzania ipo nyuma kulinganisha na baadhi ya nchi nyingine jirani kwa suala la kiasi na ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kupelekwa nje.
Amesema, uongezaji wa thamani na ubora wa utengenezaji bidhaa na mazao bado umejikita katika sekta chache na kuifanya Tanzania iwe katika hatari ya ushindani wa masoko ya kimataifa.
“Chakula na vinywaji pekee ndivyo vinavyochangia karibu nusu ya usindikajii ulioongezwa thamani (value addition), wakati bidhaa za kilimo zina uongezaji wa thamani mdogo hivyo lipo hitaji la kubadilisha uchumi wetu kwa sekta zenye kulenga zenye uchumi mdogo ili zilenge kwenye uchumi mkubwa na kuongeza thamani ya bidhaa (value addition).
“Hivyo Watanzania wajue tu kwamba, teknoljia ya nyuklia inao mchango katika lengo hili katika mazao ya kilimo na mengineyo. Soko la kuhifadhi mazao na chakula duniani linakua kwa kiwango cha ukuaji wa kila mwaka wa karibu asilimia 4.8 katika muongo mmoja ujao kufikia takriban dola milioni 232.5 ifikapo 2025,” amesema Abel na kuongeza kuwa:
“Lengo kubwa la kutumia teknolojia hii ni kuondoa changamoto za kuongezeka kwa magonjwa yanayosababishwa na vijidudu na uharibifu mkubwa wa mazao na bidhaa kabla ya kufikia mlaji ni moja ya vigezo ambavyo teknolojia hii inapewa nafasi katika kuchangia kutatua,,” amesema Abel na kuongeza kuwa:
“Takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 30 ya vyakula duniani vinaharibika kila mwaka kwa sababu ya kuharibiwa na vijidudu au kuoza,” amesema.Â