28.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 30, 2023

Contact us: [email protected]

PURA yaingia mikataba 11 ya uzalishji wa mafuta na gesi asilia

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MAMALKA ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA) imesema hadi sasa imeingia mikataba takribani Makampuni 11 kati ya hayo Makampuni matatu yapo katika uzalishaji wa mafuta na gesi asilia.

Pia amesema katika Makampuni hayo 11 kampuni moja ni la wazawa wa ya kitanzania ambao yanawekeza katika uzalishaji wa sekta hiyo ya mafuta na gesi asilia.

Akizungumza katika Maonyesho ya 45 ya Kimatafa ya Biashara DITF
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA), Mhandisi Charles Sangweni amesema mwaka 2010,Pura ilifikia hadi Makampuni 27 lakini ilipofika mwaka 2014 bei ya mafuta ilishuka sana huku Makampuni mengi yaliondoka.

Amesema kila mkataba unaoingia na PURA,ni lazima TPDC iipitie kwani ni mbia hivyo uzawa wao unadhibitisha kupitia TPDC,

“Pamoja na hayo tunachokifanya kwetu , Makampuni yaliyopo katika mikataba sio watekelezaji wa shughuli zote za utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwahiyo zipo kampuni nyingine zinazoshiriki kuchimba kwenye kulisha wachimbaji,ulinzi,usafiri,Mawasiliano na hayo yote ni Makampuni ya kitanzania,”amesema

Amesema fursa zilizopo katika tasnia hiyo ya Mkondo wa juu zinasimamia kupitia sheria ,Miongozo na kanuni, lakini vyote hivyo havitoshi katika usimamizi hadi kuonana na watu wanaosimamia na shughuli hizo ili kuwapa maelezo ya kina juu ya shughuli wanazozifanya na Mamlaka hiyo.

“Kupitia maonesho haya tutawapa maelezo mazuri namna gani anaweza akaja na akatuona au kuingia katika mitandao yetu ili ajue fursa gani ambazo anaweza wakachukua,”alisema na kuongeza

“Hapa nchini kuna rasiliamali nyingi katika shughuli ya utafutaji inamambo mengi hivyo kunafursa mbalimbali za ajira,chakula,usafirishaji hivyo hata mtu akiwa mwenyewe anaweza akapata nafasi katika kupata fursa,”amesema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,198FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles