23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Wafanyabiashara Kagera, Uganda na Kenya watakiwa kutumia fursa

Na Nyemo Malecela, Kagera

WAFANYABIASHARA kutoka mkoani Kagera, nchini Kenya na Uganda walioshiriki maonyesho ya 21 ya biashara ya sabasaba yaliyofanyika mjini Bukoba mkoani Kagera wametakiwa kutumia fursa zinazopatikana nchi Tanzania kukuza wigo wa kibiashara na kuboresha mahusiano ya nchi hizo.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Moses Machali alipotembelea maonyesho ya sabasaba na kuzungumza na wafanyabiashara kutoka nchini Kenya, Uganda na Tanzania walioshiriki walioleta bidhaa zao katika maonyesho hayo.

“Kagera ina fursa nyingi za kibiashara kwa kuwa makutano ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jambo ambalo linasababisha kuwa soko kuu la bidhaa zinazopatikana katika nchi hizo, lakini pia una bidhaa nyingi zinazopatikana mkoani humo na hazipatikana nchi nyingine au mikoa mingine kama vile senene,” alisema Machali.

Machali alisema ili kuboresha mazingira ya kufanyia biashara katika maonyesho hayo atashirikiana na ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati, Steven Byabato kuhakikisha unawekwa umeme katika eneo lililotengwa maalumu kwa ajili ya maonyesho hayo.

“Kutokana na ushiriki mkubwa wa wafanyabiashara kutoka nchini Tanzania, Kenya na Uganda eneo hili la wazi ambako yanafanyika maonyesho haya kwa sasa ni dogo hivyo halitoshi ndio maana serikali ya Mkoa wa Kagera imetenga eneo lingine la wazi ambalo ni pana litakalosaidia wafanyabiashara kushiriki kwa wingi na kuweka miundombinu ya kudumu kwa ajili ya kukuza uchumi wao.

Eneo hili  la viwanja vya jengo la Chama Cha Mapinduzi (CCM) linalotumiwa kwa sasa halikidhi lengo la mshiriki kwani ni finyu na haliruhusu baadhi ya bidhaa za kiteknilojia kuwepo ambazo zingewasaidia wafanyabiashara wengi kujifunza zaidi,” alisema Machali.

Alisema kupitia uongozi wa Mkoa wa Kagera na Jumuiya ya Wafanyabiashara wataongea na Byabato ili eneo jipya lililotengwa liweze kupata umeme kwa haraka na wafanyabiasha na wajasirimali watashika maeneo ya kuweka miundombinu ya kufanyia shuguli zao za kibiashara.

Aidha Machali alisema maonyesho ya sabasaba hayalengi kuuza bidhaa zinazoonyeshwa kwenye mabanda pekee bali wapo wanaofika kuangalia ili waweze kujifunza jinsi ya kusindika na kuandaa eneo la bidhaa.

Naye Katibu Mtendaji wa Uratibu wa maonyesho hayo mkoani Kagera (KAIDEP), Deogratius Kajua alisema changamoto kubwa inayojitokeza katika uandaaji ni eneo kuwa dogo ukulinganisha na washiriki wanaofika hapo kutoka nchi ya Congo, Rwanda, Uganda na Kenya na wenyeji wa mkoani Kagera.

Alisema lengo la kuratibu maonyesho hayo ni kusaidia washiriki kutangaza bidhaa zao kwani mkoa huo umepakana na nchi za Afrika Mashariki ambao uleta baadhi zao kila mwaka katika eneo hilo.

Aliongeza kwa hatua za awali za kuweza kupata eneo kubwa la kufanyia maonyesho hayo zimekamilika baada ya jumuiya ya wafanyabiashara mjini humo kupatiwa eneo katika kijiji cha Mwanzomgumu lilipo wilayani Misenyi mkoani humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles