25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

TACAIDS, ATF zakutana kujadili Mkakati wa Taifa wa tano wa Kudhibiti UKIMWI – NMSF V

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imefanya kikao cha pamoja na Kamisheni ya Tume hiyo na Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (ATF) ili kujadili Mkakati wa Taifa wa Tano wa Kudhibiti UKIMWI (NMSF V) ikiwa ni hatua ya kukusanya maoni ya viongozi hao wakati wa uandaaji wa mkakati huo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (ATF), Carorine Mdundo akifafanua umuhimu wa umuhimu wa kuainisha afua zinazotekeleka katika Mkakati wa Taifa wa tano wa Kudhibiti UKIMWI (NMSFV).

Akifafanua lengo la Kikao hicho kilichofanyika Juni 21, 2022 jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Lenard Maboko amesema kikao hicho ni muhimu kwa kuwa hivi sasa wapo katika maandalizi ya Mkakati wa Tano wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, ambao huo ndio mwongozo wa kitaifa katika utekelezaji wa shughuli za UKIMWI.

“Sababu za kuandaa mkakati huu ni kuendena na mikakati ya ndani na ile ya Kidunia ikiwa ni pamoja na Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI la mwaka 2020/2021, Mkakati wa Dunia wa UKIMWI (GIS) na Mkakati wa Sekta ya Afya na Sera ya Sekta ya Afya ya Mwaka 2020.

“Hivyo kikao hiki ni muhimu kwa kuwa hivi sasa tupo katika maandalizi ya Mkakati wa Tano wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, ambao huo ndio mwongozo wa kitaifa katika utekelezaji wa shughuli za UKIMWI,” amesema Dk. Maboko.

Nae Mwezeshaji Kiongozi wa mkakati huo, Dk. Emmanuel Matechi amesema mkakati wa tano umeainisha sekta zote kuja pamoja katika msukumo wa pamoja kuhakikisha kila moja inachangia katika jitihada za kumaliza UKIMWI ifikapo 2030.

“Mkakati huu tunahitaji sekta zote zije pamoja katika kumaliza UKIMWI,hivyo sekta zote zinahitaji msukumo wa pamoja katika utekelezaji na mkakati huu unaonesha kila sekta itafanya nini katika utekelezaji au inachangia vipi katika kumaliza UKIMWI,” amesema Dk. Matechi.

Picha ya Pamoja ya Washiriki wa kikao cha kujadili Mkakati wa Taifa wa Tano kilichofanyika Juni 21, 2022 jijini Dar es Salaam.

Aidha, ameainisha baadhi ya maeneo ya vipaumbele vya mkakati wa tano kuwa ni maambukizi mapya, matibabu, upimaji, kuondoa maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto,kuondoa vikwazo pamoja na kutokuwa na usawa, kuwa na uhakika na huduma zetu zikisaidiwa na Mipango au Mifumo Imara pamoja na kuimarisha na Utendaji wetu na uhakika wa raslimali pamoja na ufatiliaji na tathimini.

Dk. Matechi amefafanua kuwa mkakati huo umeainisha maeneo mengine yaliyozingatiwa  kuwa ni kuangalia wachache waliobaki nyuma kutokana na jiografia pamoja na baadhi ya makundi yao wapewe kipumbele (Geographical na population pritization),ikiwa na pamoja na umuhimu wa kuzirudisha sekta zote katika utekelezaji wa afua za kuondoa maambukizi au kudhibiti UKIMWI pamoja na Kumwangalia mgonjwa au mtu anayepokea huduma kwa ujumla na kumpa huduma zote pia Kuhakikisha kwamba lazima turuhusu jamii iongoze utekelezaji wa kimkakati.

Upande wao Wajumbe wa Bodi ya ATF na Kamisheni ya wakijadili Mkakati huo wamesema jitihada zimefanyika katika uandaaji wa mkakati huo japo yapo mapungufu madogo ambayo yanahitaji kufanyiwa mrekebisho ikiwa ni pamoja na kuongoza eneo la uraghibishi kwa uapande wa viongozi wa dini, afua ya mabadliko ya tabia pia ni muhimu ionekane katika mkakati huu.

Aidha, wamewapongeza wataalam walioandaa mkakati huo pamoja na kuwaagiza kuongeza michango yao walioitoa ambayo inalenga kuongeza ubora wa mkakati huo, ikiwa ni pamoja na kuingiza afua zinazotekelezeka au zile ambazo zina uwezekano wa kupata fedha za utekelezaji na hiyo ichukuliwe kwenye rejea ya mkakati uliopita kuwa ni ngapi zimetelezeka na ngapi hazikutekelezeka na kuainisha sababu ikiwa  lengo ni kusaidia kupunguza kuweka afua zisizotekelezeka.

Kikao hicho pia kiliudhuriwa na Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI, Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (ATF) pamoja na baadhi ya Sekretarieti ya TACAIDS. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles