21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao kusaidia huduma za uzazi nchini

Na WAF – Dodoma

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel kwa niaba ya Waziri Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao akiwemo, Steven Nyerere na Vyonne Cherrie (Monalisa) katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Pamoja na mambo mengine walijadiliana kuhusu malengo ya taasisi hiyo kuhakikisha kwamba afya ya mama na mtoto inaboreshwa hasa katika kipindi kigumu cha mama kujifungua.

Viongozi hao wamesema taasisi hiyo imeamua kujikita katika eneo la afya ya mama na mtoto baada ya kufanya utafiti mdogo katika mikoa ya nyanda za juu kusini pamoja na ukanda wa kati na kujiridhisha kuwa eneo hilo linahitaji ufumbuzi na usimamizi wa karibu.

Kwa mantiki hiyo, Viongozi hao wamesema taasisi hiyo kupitia washirika wameanzisha kampeni iitwayo “Jali afya ya mama na mtoto” ambapo itasaidia maboresho katika maeneo muhimu ikiwemo ujenzi wa zahanati, ununuzi wa vifaa tiba kama vile Ultra Sound pamoja na vifaa vyote vinavyohusu afya ya na mtoto.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Dk. Mollel ameishukuru taasisi hiyo kwa kusaidia jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za afya nchini hasa afya ya mama na mtoto na amesema Wizara ya Afya iko tayari kutoa ushirikiano mkubwa katika kutekeleza malengo ya taasisi hiyo ikiwemo kutoa taarifa kamili ya maeneo yenye upungufu wa huduma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles