27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 149,537 kupewa nyandarua Songwe

Na Denis Sikonde, Songwe

WANAFUNZI 149,537 wa shule za msingi mkoani Songwe wanatarajia kunufaika na mpango wa ugawaji vyandarua bure lengo likiwa ni kupunguza maabukizi ya ugongwa wa Malaria ambapo kwa mkoa huo maambukizi yapo chini ya 1%.

Hayo yamebainishwa Juni 28, na Mkuu wa Mkoa huo, Omary Mgumba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ugawaji wa vyandarua kwa shule za msingi mkoani humo uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa eneo la Nselewa wilayani Mbozi.

Mgumba amesema katika kampeni hiyo wanatarajia Julai 4, 2022 ambapo wanafunzi watakaonufaika ni kuanzia darasa la kwanza mpaka darasa saba na kwamba kabla ya kuanza utekelezaji wa kampeni hiyo mkoa utashirikiana na wizara ya afya na ile ya TAMISEMI sambamba na wadau muhimu wakiwepo viongozi wa taasisi zisizo za serikali na zisizo za serikali, viongozi wa dini na mila ili kuifikia jamii kiurahisi kutoa elimu juu ya kampeni hiyo.

Mgumba amesema kila shule ya msingi ndani ya mkoa huo katika wilaya za Ileje, Momba, Songwe itapatiwa vyandarua na kuwasihi walimu watakaopewa dhamana yakusimamia ugawaji huo wagawe kwa kila mwanafunzi na si kugawa kwa masilahi yao binafsi huku akisema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaokiuka taratibu za kampeni hiyo.

“Tumeamua kuanza na watoto wa shule za msingi kwa sababu hawa ndiyo watu wazima wa kesho, hivyo tukiwajengea utamaduni wa matumizi sahihi ya vyandarua itajengeka kuwa tabia yao  kumbe wataendeleza hata watakapokuwa na maisha yao ya kujitegemea,” amesema Mgumba.

Mgumba ameongeza kuwa katika utafiti uliofanyika mwaka 2017 ulionyesha kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa mkoa wa Songwe ipo chini ya asilimia 1 ambapo kwa kitaifa ni asilimia 7 huku akiwasihi wananchi kuendelea kuchukuaa tahadhari juu ya ugonjwa huo.

Amesisitiza kuwa lengo la serikali ni kudhibiti ugonjwa wa malaria hadi kufikia asilimia 3 ifikapo mwaka 2025 na kufikia mwaka 2030 kuutokomeza kabisa nakwamba ndiyo sababu serikali imeanza zoezi la ugawaji wa vyandarua kupitia makundi mbalimbali ikiwepo wanafunzi ambao watakuwa watu wazima baadae.

Ni marufuku…

Hata hivyo, Mgumba amepiga marufuku wananchi kutumia vyandarua kama nyavu za kuvulia samaki na matumizi mengineyo tofauti na kujikinga na ugonjwa wa malaria nakuonya kuwa atakaebainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Mwakilishi wa wizara ya afya kitengo cha Kudhibiti Malaria, Peter Gitanya amesema usambazaji wa vyandarua hivyo utafanywa na Bohari Kuu ya Dawa(MSD) kwenda ngazi ya shule za msingi huku, akisema katika kampeni hiyo ni mwendelezo na kwa Tanzania Bara wanafunzi wa shule za msingi milioni 1,495,551 wanatarajia kunufaika na ugawaji wa vyandarua.

Gitarya pia amewatahadharisha walimu kutojihusisha na wizi wa vyandarua hivyo na kuwasihi wazazi na walezi kutouza vyandarua ambavyo vimegawiwa na wizara ya afya kwa lengo la kutokomeza ugonjwa huo kufikia mwaka 2030.

Nae, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dk, Bonifasi Kasululu amesema wananchi wanatakiwa kuendelea kushirikiana na wataalamu wa afya kila mtu kwa imani kutoa elimu ya kampeni ya ugawaji wa vyandarua sambamba na kugawa kuvigawa kwa wakati pindi vitakapogawiwa shuleni.

Kwa upande wake, Yonas Alfred akizungumuza kwa niaba ya wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo amewaomba wakazi wa mkoa huo kwa ujumla kuunga mkono na kuzingatia elimu ya matumizi sahihi ya vyandarua inayotolewa kwa wanafunzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles