24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi ya Kikwete yaokoa bilioni 5/-  

Dk. Peter KisengeNA HADIA KHAMIS, DAR ES SALAAM

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeokoa Sh bilioni tano kwa watoto 64 waliofanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa moyo.

Idadi kama hiyo ingeigharimu serikali kiasi hicho cha fedha kwa kuwapeleka wagonjwa kutibiwa India.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkuu wa Kitengo cha Tiba ya Magonjwa ya Moyo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya moyo, Dk. Peter Kisenge alisema timu ya wataalamu 35 kutoka nchi mbalimbali wanaendelea kuwafanyia upasuaji watoto wenye tatizo la moyo.

Alisema hakuna mtoto hata mmoja aliyefariki dunia  jambo linaloendelea kuwatia nguvu na kutoa matumaini mapya kwa madaktari bingwa hao wa kuendelea kufanya upasuaji.

“Tunalishukuru pia gazeti la Mtanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha jamii kuendelea kujitokeza katika suala zima la uchangiaji damu wa hiari kwa watoto wenye matatizo ya moyo,” alisema.

 

Wakati huohuo, Hospitali ya CCBRT jana ilikabidhi vifaa vya kusaidia mtoto kuweza kupumua baada ya kuzaliwa.

Msaada huo una thamani ya Sh milioni 50.

Mkurugenzi wa CCBRT kitengo cha Mama na Mtoto, Suzan Boon alisema msaada huo ni moja ya ushirikiano baina Muhimbili na Hospitali ya CCBRT yenye lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga na mama mjamzito.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles