24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Taarifa za michezo kutoka majuu

Hassan Daudi na Mitandao

Neuer, Muller wamlilia kocha
MASTAA wa Bayern Munich, Manuel Neuer na Thomas Muller, wamekerwa na namna klabu hiyo ilivyoshindwa kumaliza bifu kati ya kocha wao, Hansi Flick, na mkurugenzi wa michezo,  Hasan ‘Brazzo’ Salihamidzic.

Uhusiano mbovu kati ya Flick na Salihamidzic limesabisha kocha huyo asema ataondoka zake mwishoni mwa msimu huu, uamuzi ambao umemuhuzunisha nahodha Neuer na msaidizi wake, Muller.

Kwa upande mwingine, inasemekana kuwa wawili hao wanatamani kuona Flick akipewa timu ya taifa ya Ujerumani ili waendelee kufanya naye kazi.

Milan nayo kujitoa ESL

AC Milan iko mbioni kuwa klabu ya kwanza ya Italia kujiondoa kwenye michuano mipya ya European Super League (ESL).

Milan ilikuwa sehemu ya klabu 12 zilizotangaza utayari wake wa kushiriki michuano hiyo iliyotambulishwa wikiendi iliyopita.

Mashindano hayo yaliyotambulishwa wikiendi iliyopita, yanapingwa vikali na tayari klabu sita za England zimeshatangaza kujitoa.

Beki Senegal kocha mpya Ufaransa

ALIYEKUWA beki wa Newcastle United na timu ya taifa ya Senegal, Habib Beye, anatarajiwa kupewa kibarua cha kuinoa Angers SCO ya Ufaransa.

Beye anamalizika kozi yake ya BEPF ambayo ndiyo kubwa zaidi kwa kocha kuweza kuifundisha timu yoyote Ligi Kuu nchini humo (Ligue 1).

Bellerin aisubiri PSG

ARSENAL wameanza harakati za kumtafuta mrithi wa Hector Bellerin kwani Mhispania huyo anataka kwenda Ufaransa anakotakiwa na PSG.

Kwa mujibu wa gazeti la Sport la Hispania, kuna uwezekano mdogo wa kumuona Bellerin akiwa na uzi wa Arsenal msimu ujao.

Wakati huo huo, bado mchezaji huyo hajaonesha kupotezea ofa ya kurudi nyumbani, Hispania, anakowindwa na Barcelona.

Aguero ataja klabu anayokwenda

IMERIPOTIWA kuwa Sergio Aguero ameshaitajia familia yake klabu atakayokuwa msimu ujao.

Hayo yanaibuka huku tetesi za Aguero kwenda Barcelona zikiendelea kutikisa huko mitandaoni.

Sasa, mfungaji bora huyo wa muda wote wa Man City amewambia ndugu zake kuwa atakipiga Nou Camp msimu ujao.

Neville: Glazer tuachie City yetu!

LEJENDARI wa Manchester United, Gary Neville, ameitaka familia ya Glazer inayomiliki klabuni hapo kuondoka mara moja.

Kauli hiyo ya Neville inatanguliwa na ile ya Makamu Mwenyekiti wa Man United, Ed Woodward, kujiuzulu.

Ed Woodward aliachia ngazi baada ya Man United kujitoa kwenye mpango wa kushiriki European Super League (ESL).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles