24.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 15, 2024

Contact us: [email protected]

TAARIFA ZA KUKAMWATA MASOUD KIPANYA ZASHTUA


Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

NI mshtuko. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kuenea kwa taarifa za kukamatwa kwa mchora katuni mashuhuri nchini, Masoud Kipanya.

Taarifa hizo zilianza kusambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii jana jioni, huku kundi kubwa la Watanzania likijikuta likihoji usahihi wa taarifa hizo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Kipanya alidaiwa kukamatwa akihusishwa na tuhuma za uchochezi kutokana na baadhi ya michoro yake.

MTANZANIA ilipojaribu kumtafuta kwa simu yake ya kiganjani, iliita kwa muda mrefu bila kupokewa na baada ya muda ilizimwa kabisa jambo ambalo lilizidi kuzua hofu.

Kipanya ambaye pia ni mwanahabari, mtangazaji wa Clouds Media Group, ilielezwa kwamba muda mwingi wa jana alikuwa nyumbani kwake na familia yake kabla ya taarifa za kudaiwa kukamatwa.

“Hatujathibitisha juu ya yeye kukamatwa, hapatikani kwake, mke wake alimwacha nyumbani aliporudi hakumkuta,” alisema mmoja wa viongozi wa Clouds Media ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini kwa kuwa si msemaji wa kampuni.

Kutokana na taarifa hiyo, MTANZANIA ilijaribu tena kumtafuta Kipanya kwa simu yake ya kiganjani na iliita tena bila kupokewa na baada ya muda ilizimwa na kutopatikana tena hewani.

 POLISI

MTANZANIA ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, kupata ufafanuzi wa tukio hilo, alisema……………………..

Kwa habari zaidi usikose kununua nakala yako ya MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles