23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

SWEDEN YAIPA TANZANIA SH BILIONI 435

Mwandishi wetu

SERIKALI ya Sweden imeipa Tanzania fedha za Sweden SEK. Bilioni 1.64 (Sh bilioni 435.79) kwa ajili ya msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu.

Makubaliano ya msaada huo yamesainiwa jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James na Mkuu wa Kitengo cha  Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini, Ulf Kallsting.

James akizungumzia tukio hilo, alisema  imesainiwa mikataba mitatu ya msaada huo ambayo ni, mkataba kwa ajili ya kusaidia bajeti ya Serikali wa Sh bilioni 159.59   kwa kipindi cha 2017/18 hadi 2019/2020, ambapo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Sh  bilioni 53.20 zitatolewa.

Alisema fedha hizo zitaelekezwa katika kuboresha uhalisia wa bajeti ili kuweza kutimiza majukumu ya kisera, kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ya kikodi na yasiyo ya kodi na kusaidia Serikali kutoa huduma nzuri kwa wananchi kupitia taratibu za manunuzi.

Mkataba mwingine ni kwa ajili ya kusaidia Mpango wa Elimu kwa Matokeo (EPforR) wa Sh bilioni 235.40 kuanzia mwaka 2017/18 hadi 2020/2021.

 

“Baada ya ya Serikali kutimiza wajibu wake wa kupeleka fedha katika Sekta ya elimu kwa wakati, wameamua kutupatia fedha hizo ambazo Serikali tunazipangia kazi kulingana na vipaumbele”, alieleza James.

Alisema Mpango wa Elimu kwa Matokeo ulianza mwaka 2015/2016 na katika kipindi hicho yamepatikana maendeleo katika ujenzi wa miundombinu ya madarasa, vyoo, mabweni. Utekelezaji wake umefanywa katika shule 361 kwenye Halmashauri 129 nchini.

“Katika mpango huo vyuo 17 vya Walimu vimekarabatiwa ikiwa ni pamoja na kununua Kompyuta 260,  magodoro 6,730 na viti 1,976,” alisema James.

Mkataba wa tatu uliosainiwa ni wa Marekebisho ya Mkataba wa  Mpango wa Kusoma, Kuhesabu na Kuandika wenye Dola za Marekani 94.8 zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Global Partnership for Education (GEP) na kukabidhiwa kwa nchi ya Sweden ili iweze kuusimamia.

Alisema Serikali ilisaini mkataba  huo na Sweden Mei, 2015 na muda wa utoaji wa fedha hizo ulikwisha Agosti, 2016 na kubakia kiasi cha dola milioni 18.3 ambazo zitapatikana baada ya kusainiwa kwa mkataba huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles