30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Sungusungu kutumika kukabili uvuvi haramu

uvuvi-haramuNa PETER FABIAN

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ameanza jitihada za kufufua Sungusungu watumike kupambana na uvuvi haramu ndani ya Ziwa Victoria.

Alisema lengo ni kuutokomeza uvuvi huo unaoathiri taifa na maliasili.
Alikuwa akizungumza katika kikao cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) cha Halmashauri Kuu ya Mkoa wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020.

Mongella alisema uongozi unajipanga kufufua Sungusungu wasaidiane na vyombo vya dola katika kuwabaini, kuwakamata wahalifu wanaojihusisha na uvuvi haramu katika maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria.
Alisema wimbi la uvuvi haramu bado ni kubwa na kuonekana na baadhi ya wavuvi kubuni mbinu mpya ya kunasa samaki.

RC alisema wengine hutumia vumbi la pumba za mpunga kwa kumwaga ziwani na samaki wanapokula na kunywa maji huvimbewa, kufa na kuibuka juu njia ambayo ni hatari kwa vile huua hadi vifaranga.

“Kuna wavuvi wamebuni mbinu mpya ya uvuvi haramu, wanakuja mijini kununua pumba za mpunga na kwenda kutumia vijana kumwaga pumba hizo ziwani.

“Kisha wao huenda kuokota samaki waliokufa na kuzagaa maeneo hayo. Ingawa kitaalamu haina madhara kwa watumiaji samaki lakini njia hii inaua hadi vifaranga vya samaki,” alisema.

Alisema kwa kuwa polisi na maofisa uvuvi hawawezi kufika kila eneo kwa wakati mmoja wamefikiri namna ya kuimarishwa ikiwa ni pamoja na kufufuliwa jeshi hilo la jadi lisaidie vita hii ya kupambana na uvuvi haramu.
Mongella aliipongeza Wilaya ya Sengerema pekee kuwa ndiyo inayoonekana kuweka utaratibu mzuri wa kupambana na uvuvi haramu.

Alisema katika hatua hiyo hushirikishwa viongozi wa maeneo husika wakiwemo madiwani wa kata.
RC aliziagiza wilaya nyingine ziige wilaya hiyo katika kukomesha uvuvi harama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles