AnnaPotinus, Dar es salaam
Rais John Magufuli amesema mradi wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge umebarikiwa na Mwenyezi Mungu kwa kukutanisha viongozi wengi wa dini na kwamba utaleta manufaa makubwa nchini.
Amesema hayo leo Jumatano Desemba 12, katika hafla ya kusaini mkataba waujenzi wa mradi huo na Serikali ya misri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini nchini.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria katika hafla hyo ni pamoja na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, Nabii wa Kanisa la Efatha, Josephat Mwingira, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo (Mzee wa Upako) na wengine wengi.
“Haijawahi kutokea mradi ukasainiwa na viongozi wa dini wengi kiasi hiki maana yake ni wa kipekee na umebarikiwa na Mwenyezi Mungu hivyo nina imani sana utafanikiwa,” amesema.
Wakati huo huo rais Magufuli ametaja vipaumbele walivyotumia wakatiwakitafakari ni chanzo gani kingefaa zaidi katika kukamilisha mradi huo ambao utasaidia kupata umeme wa uhakika na wa bei rahisi lakini pia utapunguza uharibifu wamazingira nchini
“Baada ya kutafakari ni chanzo gani kinatufaa kwa kufuata mambo manneambayo ni uhakika wa chanzo, gharama za utekelezaji, gharama za uendeshaji pamoja na tija ndipo tuliona kuwa mradi huu unatufaa zaidi,” amesema.