27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Steve Nyerere ateuliwa Balozi wa Uviko-19

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Msanii maarufu nchini na Mwenyekiti wa Jukwaa la Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ ameteuliwa kuwa Balozi wa harakati za kupambana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (Uviko 19).

Steve ameteuliwa leo Alhamisi Agosti 12 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Steve, wengine walioteuliwa ni Mwanaharakati wa Kutetea Haki za Wanawake nchini, Joyce Kiria na Mbunge wa Viti Maalumu, Neema.

Tangu janga la Uviko 19 liibuke tena nchini mwaka huu, Steve ameonyesha kupambana na janga hilo huku akihamasisha Watanzania kupata chanjo ili kujikinga dhidi ya ugonjwa huo hatari duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles