22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Ubakaji wenye matatizo ya akili Kilimanjaro chanzo watoto mtaani

Na Upendo Mosha,Moshi

ONGEZEKO la vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji wa wanawake wenye matatizo ya akili(vichaa),mkoani Kilimanjaro, imetajwa kuwa sababu inayochangia uwepo wa watoto wa mitaani.

Kutokana na hali hiyo,jamii imetakiwa kujiwekea utamaduni ya kusaidia kulea watoto wanaotoka katika mazingira magumu badala ya kutegemea asasi za kiraia, mashirika binafsi na serikali pekee kubeba jukumu hilo.

Hayo yamebainishwa na rais wa taasisi ya New life Foundation,inayojishughulisha na kusaidia watoto wanaotoka katika mazingira magumu, Glorious Shoo, wakati akizungumza na waandishi wa habari,mjini Moshi,mkoani Kilimanjaro, juu ya mafanikio na changamoyo ya miaka 20 toka kuanzishwa kwa tasisi hiyo hapa nchini.

Amesema kwa sasa kumekuwa na vitendo vingi vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kubakwa na kupewa ujauzito wanawake wenye matatizo ya akili jambo ambalo limekuwa likisababisha ongezeko la watoto wengi wa mitaani ambao hukosa malezi bora ikiwemo elimu.

“Kwa miaka 20 shirika letu limekuwa likiwasaidia watoto wengi hususani wale wanaotoka katika mazingira magumu kwa maana ya watoto wa vichaa,watoto wanaotoka katika jamii za wafugaji,Waadzabe na Wasonjo,lakin tatizo kubwa ni watoto wengi ni wa vichaa ambao hupewa ujauzito na kutekeleza watoto mitaani”alisema Shoo

“Watoto wa wanawake ambao ni vichaa wamekuwa wengi mtaani na sasa inaonekana ni tatizo ambalo linakuwa taratibu,watoto hawa ni wajamii hawana msaada mwingine,jamii ijifunze kujitolea kusaidia watoto wa aina hii iwasaidie isituachie jukumu hili sisi pekee na serikali”amesema

Aidha amesema shirika hilo limekuwa likiwasaidia watoto hao kwa kuwalea na kuwasomesha katika shule zinazomilikiwa na taasisi hiyo kwa kuwatafutia wafadhili kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi.

“Asilimia 70 ya watoto wanaosoma katika shule zetu za Fountain of Hope msingi na sekondari wanaotoka katika mazingira magumu ambao wengi wao ni watoto wa vichaa huwa tunawatafutia ufadhili na wanasoma kwa ajili ya kuwasaidia kutimiza ndoto zao lakini asilimia 30 ni watoto wa watu wenye uwezo na wanalipa ada kawaida”amesema

Shoo,amesema pamoja na mafanikio makubwa waliyoyapata katika kuhudumia jamii kwa miaka 20 bado wanakabili na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa fedha za kujiendesha na kuiomba serikali kuangalia namna ya kusaidia taasisi zinazofanya huduma hizo kwa kuwapa ruzuku.

Marthin Hamisi,ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne, amesema yeye alitokea katika jamii ya kabila la Wadzabe ambapo taasisi hiyo ilimsomesha kuaanzia ngazi ya chekechea,msingi na sasa Sekondari na kwamba anategemea kutimiza ndoto zake na kujitokeza kwenda kuisaida jamii yake kuona umuhimu wa elimu.

Naye Castory Tarimo,amesema amenufaika na taasisi hiyo baada ya kusaidia kutokana na mzazi wake kuwa na matatizo ya akili ambapo alishindwa kuwalea na kwamba anamategemeo makubwa ya kutimiza ndoto zake,ambapo aliniomba jamii kutoa msaada wa kusaidia watoto wanaotoka katika mazingira magumu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles