23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Steve Nyerere ‘amtuliza’ Nondo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mwenyekiti wa Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengere maarufu, Steve Nyerere amjia juu Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo, Abdul Nondo kwa kuitisha maandamano na kusisitiza kwamba Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) inafanyiwa kazi na Serikali.

Steve ameyasema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Meya wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam alipofika kwa ajili ya kutoa msaada kwa watoto wenye uhitaji katika vituo mbalimbali vilivyopo wilayani humo.

Ikumbukwa kuwa Jumanne Aprili 18, 2023 Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam lilizuia maandamano yaliyokuwa yaanzie kwenye ofisi za makao makuu ya ACT zilizopo Magomeni yakiongozwa na Nondo.

“Kuandamana ni ushamba, nchi ya leo ya Tanzania mtu akiandamana ni ushamba watu wanakaa chini ndio maana hata kiongozi wao wamekaa chini, sasa huyu kijana katokea wapi kuandamana na ukiandamana ni kukosa shughuli,” amesema Steve.

Pia aliongezea kuwa Nondo anatakiwa kutulia na kuachia viongozi wa Serikali kuifanyia kazi ripoti ya CAG na kuwataka Watanzania kupuuzia maandamano hayo kwani nchi ni tulivu na kuiachia serikali kufanya kazi yao.

Awal, kwa mujibu wa Nondo, maandamano hayo ya amani yalipangwa kuanzia Manzese hadi Ikulu kuonana na Rais Samia Suluhu Hasaan na kumfikishia ujumbe wa kutokukubaliana na ubadhilifu wa fedha za umma uliofanywa, kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ya kila mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles