24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Sterling: Nilifurahi Liverpool kutwaa Ligi ya Mabingwa

YOKOHAMA, JAPAN

KIUNGO mshambuliaji wa Manchester City, Raheem Sterling amesema alifurahi kuona klabu yake ya zamani ya  Liverpool ikishinda taji la Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.

Liverpool ilitwaa taji hilo, baada ya kuichapa Tottenham Spurs bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Wanda Metropolitano Madrid, Hispania .

Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, alisema kuwa Manchester City kushinda taji la Ligi Kuu England ilikuwa muhimu zaidi.

Sterling aliondoka Merseyside mwaka 2015  na kujiunga na Man City katika hali ambayo iliwachefua mashabiki wa Liverpool kutokana na nyota huyo kulazimisha kuondoka katika kikosi chao, akiwa mchezaji muhimu.

“Nilifurahishwa sana na wao kushinda taji hilo, nimefurahi baadhi ya  wachezaji ambao kuchukua ubingwa  Ligi ya Mabingwa, ni jambo  kubwa kwetu, lakini jambo letu muhimu zaidi ni kushinda Ligi Kuu hilo ndilo lengo letu kuu kuelekea msimu ujao.

“Ndiyo, itakuwa vizuri kushinda Ligi ya Mabingwa lakini kwanza tunataka kushinda ligi.Ligi Kuu ni mkate na siagi yako, kila wikiendi unajifunza kitu kipya , Ligi ya Mabingwa ndiyo inayoonekana vizuri na ya kifahari kama watu wanavyosema, lakini kila mwishoni mwa wiki unahama kwenda kukutana na mazingira magumu,”alisema Sterling.

 City ilishinda taji la Ligi Kuu Eng;and katika dakika za mwisho  msimu uliopita, ikimaliza msimu ikiwa na pointi 98, ikifuatiwa kwa karibu na  Liverpool iliyomaliza na pointi 97.

 
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles