24 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Stephen Masele achukua fomu za kuwania nafasi ya Spika wa Bunge

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MBUNGE wa zamani wa Shinyanga na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Mheshimiwa Stephen Julius Masele, amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Masele anawania nafasi iliyoachwa wazi na Spika wa zamani wa Bunge hilo, Job Ndugai aliyejiuzulu wiki iliyopita, huku Mbunge huyo aliyewahi pia kuwa Naibu waziri wa Nishati na Madini, amechukua fomu hiyo leo Jumatatu ya January 10, 2022 katika ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lumumba, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuchukua fomu hiyo, Masele alisema kuwa ameamua kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi ya Spika, akitumia haki yake ya msingi ya Kikatiba, akiamini anao uwezo mzuri wa kuitumikia nafasi hiyo.

“Kwa sasa sina kubwa la kusema kwakuwa sio wakati sahihi kuzungumzia vipaumbele, ila ninachoweza kusema ni namna gani nina haki zote za kuwa mgombea wa nafasi hiyo kama ilivyoelezwa kwenye sharia, kanuni na taratibu zote za chama chetu CCM.

“Nitasema baadaye dhamira yangu halisi muda muafaka utakapofika kwakuwa chama kina utaratibu wake uliowekwa ambao napaswa kuufuata nikiamini kila kitu kitakwenda vizuri,” amesema Masele.

Mbali na nafasi ya Spika wa Bunge kugombewa na wabunge, Chama Cha Mapinduzi kimeweka utaratibu mzuri wa makada wake kuchukua fomu ili kupendekezwa kuwania nafasi hiyo ambayo watu wa mwisho kupiga kura ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya taratibu zote ndani ya chama hicho kukamilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles