Stephen Curry kukosa michezo miwili

0
977

Stephen CurryNEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa kikapu wa timu ya Golden State Warriors, Stephen Curry, anatarajia kukosa michezo miwili ya Ligi Kuu ya NBA baada ya kusumbuliwa na goti.

Nyota huyo wa tuzo ya MVP msimu uliopita, ni mara ya pili kwa msimu huu kuumia ambapo awali alikuwa anasumbuliwa na goti la kulia ila kwa sasa anasumbuliwa na goti la kushoto.

Kocha wa timu hiyo, Luke Walton, amethibitisha kuumia kwa mchezaji huyo lakini bado anaamini ataendelea kufanya vizuri na kikosi chake.

“Curry atakuwa nje ya uwanja na kukosa michezo miwili, ni pigo kubwa kwa upande wetu kwa kuwa ni mchezaji ambaye ana mchango mkubwa kwetu, ila bado tuna wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa na kuisaidia timu,” alisema Walton.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Kings in Oakland, mchezaji huyo alitumia dakika 30 na kutolewa nje kutokana na maumivu anayoyapata.

“Nimepata maumivu ya goti, lakini ninaamini nitaendelea kuwa vizuri kwa ajili ya kuisaidia timu yangu, bado timu inafanya vizuri na itaendelea vizuri na kuna uwezekano wa kufanikiwa kutetea ubingwa msimu huu.

“Kuna ushindani mkubwa kwa sasa, lakini kikubwa ni ushirikiano wa hali ya juu ambao unaweza kuipa ubingwa timu,” alisema Curry.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here