20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Statoil yatoa milioni 10/- kwa shujaa

NA GLORI MLAY

MKAZI kutoka Mtwara, Yunus Mtopa, amekabidhiwa Sh milioni 10 baada ya kushinda katika shindano la Mashujaa wa Kesho lililoandaliwa na Kampuni ya Statoil.

Shindano hilo ambalo lilishirikisha vijana zaidi ya 40 kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara ambao walichujwa na kuingia 10 na baadaye tano bora na sasa ametangazwa mshindi aliyeandaa wazo la biashara ya juisi.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa, alisema ushindi huo ni hatua ya mwanzo ya kumwezesha mjasiriamali kutimiza ndoto zake.

Mtopa ni mkazi wa Masasi, Mtwara na amesema kuwa kupitia wazo lake atatengeneza ajira kwa vijana wengi katika eneo lake.

Wengine walioingia hatua ya tano bora ni pamoja na Salehe Kisunga, Aziz Doa, Edward Nkiliye pamoja na Razaki Kaondo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles