29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

….Kiungo Al Ahly aihofia

Hossam+Ashour+Al+AhlyCAIRO, MISRI

KIUNGO wa timu ya soka ya Al Ahly ya Misri, Hossam Ashour, amewatahadharisha wenzake akiwataka kucheza kwa makini mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga utakaochezwa  keshokutwa katika Uwanja wa Jeshi wa Burj Al Arab uliopo mjini Alexandria.

Mbali na kutaka kuimarishwa sehemu ya kiungo, pia amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu hiyo ili kuwapa wachezaji wapya nguvu na hamasa ya ushindi.

Akizungumza kupitia mtandao wa klabu hiyo, Ashour alisema ubora wa wapinzani wao Yanga unatokana na kikosi hicho kunolewa na kocha mwenye uwezo mkubwa pamoja na wachezaji wenye viwango vya kimataifa.

“Wachezaji wa Al Ahly walipata nafasi nzuri ya kujifunza katika mchezo wa awali dhidi ya Yanga ugenini hasa baada ya matokeo kuwa ya sare ya bao 1-1, hakika dakika 90 za mchezo wa marudiano nyumbani zitakuwa ni nyingi sana,” alisema Ashour.

Akizungumzia mchezo wa awali uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kiungo huyo alidai kuwa Yanga walikuwa na kasi ambapo walipiga mashuti yaliyolenga lango lao na kuwatibulia mipango yao uwanjani ya kutengeneza mabao.

“Kuna umuhimu wa mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo wa marudiano ili kuondoa mahudhurio hafifu katika michezo ya hivi karibuni.

“Ujio wao kwa wingi uwanjani utasaidia kuwapa wachezaji wapya ambao wanatarajia kuwepo kwenye michuano ya kimataifa nguvu na ari ya kucheza kwa kujiamini,” alisema Ashour.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles