27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Stars yasaka rekodi kwa Mafarao

Pg 31NA MARTIN MAZUGWA, DAR ES SALAAM

TIMU ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’inashuka katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaa leo kuwavaa Misri ‘The Pharaohs.

Stars iliyo kundi G inasaka rekodi nyingine ya kucheza Fainali ya Michuano ya Afrika mwakani itakayochezwa nchini Gabon.

Stars kwa mara ya mwisho kucheza fainali hizo za Afrika ilikuwa mwaka 1980, katika fainali zilizofanyika mjini Lagos, Nigeria.

Akizungumza Dar es Salaam jana, kocha mkuu wa Stars Charles Boniface Mkwasa, alisema mchezo huo utakaonza saa 10: 00 jioni una umuhimu mkubwa na ni kama fainali kwani wanahitaji ushindi ili kuweka matumaini ya kucheza fainali hizo nchini Gabon.

“Mechi hii ina  umuhimu  mkubwa sana kwetu, tunatakiwa kucheza kwa kujituma zaidi kwa kuwa tuna deni kubwa kwa Watanzania na tunatakiwa kulilipa,  tunakwenda kushinda na tunaahidi kufanya vizuri katika mchezo wa kesho (leo),” alisema.

Alisema wachezaji wake wapo katika hali nzuri japo kuna wachezaji wawili majeruhi ambayo hayawazuii kucheza ambao ni John Bocco na Thomas Ulimwengu.

Tanzania inashika mkia katika kundi G ikiwa na pointi moja  baada ya kucheza mechi mbili, ikifungwa ugenini na Misri mabao 3-0 na kutoa suluhu na Nigeria ikiwa ugenini.
Mafarao hao ambao ndio kinara wa kundi hilo ikiwa na pointi saba baada ya kucheza mechi tatu kama ilivyo kwa Nigeria yenye pointi mbili ambazo zote zimebakisha mchezo mmoja mmoja huku Stars ikisalia na michezo miwili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles