22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Stars yaenda Afrika Kusini kusaka makali

Timu ya Taifa, Taifa Stars
Timu ya Taifa, Taifa Stars

NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, imeondoka jana kuelekea Afrika Kusini kujiandaa na mchezo wake wa marudiano dhidi ya Msumbiji, utakaochezwa Agosti 3 katika Uwanja wa Zimpeto, mjini Maputo.

Stars imeondoka huku ikiahidi ushindi kwa Watanzania katika mchezo huo wa kusaka kucheza hatua ya makundi ya michuano ya Afrika, itakayofanyika mwakani nchini Morocco.

Awali Stars ilitoka sare ya 2-2 na Msumbiji katika mchezo wake wa kwanza mjini Dar es Salaam na inahitaji ushindi ili kusonga mbele.

Akizungumza na MTANZANIA jana kabla ya kuondoka, Meneja wa timu hiyo, Boniface Clemence, alisema wameitumia kambi yao ya Tukuyu kwa ajili ya kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika mechi ya awali na ndiyo maana hawakuwa na programu ya mechi ya kirafiki.

“Kambi ile ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya kufanya marekebisho ya mechi ya awali, hivyo tunakwenda kwanza Afrika Kusini kujiimarisha kidogo huku tukiwa na matumaini makubwa ya kufanya vema katika mechi yetu ya Agosti 3,” alisema.

Timu hiyo imeondoka ikiwa na msafara wa watu 19, wakiwa ni wachezaji pamoja na maofisa wa benchi la ufundi, huku washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wataungana na wenzao Johannesburg wakitokea Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles