Stara arudisha majeshi Bongo Fleva

0
923

StaraTomasikatikaPoziNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM
MWIMBAJI wa injili nchini, Stara Thomas ‘Stara’, ameamua kurudi rasmi katika muziki wa Bongo Fleva ambapo hivi karibuni anatarajia kuachia wimbo wake aliomshirikisha Banana Zoro.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Stara alisema anaimani wimbo huo uliopewa jina la ‘Nishike mkono’, utamtambulisha upya.
“Nimeamua kurudi nilipotekea, najua mashabiki zangu wengi watakuwa wakikumbukua jinsi gani nilikuwa nafanya vizuri,” alisema Stara.
Alisema wimbo huo utaweza kuonyesha jinsi gani amezaliwa na kipaji ambacho daima kitaendelea kuonekana kupitia kazi zake anazozifanya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here