29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mashabiki wamvamia Diamond Zanzibar

Diamond-PlatnumzNA FESTO POLEA, ZANZIBAR
KATIKA hali isiyotarajiwa askari wanaolinda katika Tamasha la Sauti za Busara walijikuta wakifanya kazi ya ziada kutawanya idadi kubwa ya mashabiki wa msanii, Nassib Abdul (Diamond), baada ya kumvamia walipomuona katika eneo hilo akiwa na mpenzi wake, Zari.
Mashabiki hao walimvamia msanii huyo na mpenzi wake kwa lengo la kupiga naye picha na wengine wakitaka kumsalimu kwa kumkumbatia lakini kutokana na kila shabiki kutaka kupata nafasi hiyo kwa haraka wakajikuta wakizua vurugu zilizolazimu askari kuwatawanya.
Msanii huyo alifika maeneo ya Forodhani nje ya ukumbi wa Ngome, Kongwe saa moja usiku na baada ya muda mwanamitindo, Martin Kadinda akaonekana kujumuika nao lakini baadaye ndipo mashabiki wakamgundua kwamba ni Diamond.
Baada ya vurugu hizo za furaha kutokea na askari kuwajibika, msanii huyo na mpenzi wake walielekea walipopaki gari lililowaleta wakaondoka eneo hilo huku mashabiki wakionekana kuendelea kumshangilia kwa furaha.
Kwa mujibu wa meneja wa msanii huyo, Babu Tale alisema msanii huyo yupo Zanzibar mapumzikoni na mpenzi wake na hakuna ratiba ya onyesho kwao.
“Diamond yupo Zanzibar amekwenda kutembea kula maisha na mpenzi wake Zari na hakuna ratiba ya shoo, amekwenda kupumzika tu,’’ alisema meneja huyo huku akidai kwamba msanii huyo kwa sasa bado hajapanga wimbo wa kutoa hivi karibuni.
Hata hivyo, naye mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotion, waandaaji wa tamasha la Sauti za Busara, Simai Mohammed, alisema mwakani wanatarajia kupokea maombi ya msanii, Abdul Nassib (Diamond) katika tamasha hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles