25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Stamico yaweka mikakati kuongeza mkaa mbadala

Na Yohana Paul, Geita

SHIRIKA la Madini la Taifa (Stamico) wamejidhatiti kuongeza uzalishaji wa mkaa mbadala utokanao na makaa ya mawe, ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa wa kupikia na kusaidia kuokoa raslimali za misitu.

Meneja Mahusiano wa Stamico, Geofrey Meena amebainisha hayo mbele Waziri wa Nch, Ofisi ya Makamu wa rais Muungano na Mazingira katika viwanja vya Maonyesho ya Tano ya Teknolojia ya Madini.

Amesema walianza kwa kuzalisha mkaa wa majaribio na umeonekana kuwa na ufanisi mkubwa ikilinganishwa na mkaa wa miti na mkakati ipo hatua za mwisho kuimarisha upatikanaji wa mkaa huo mjini na vijijini.

Akifafanua mradi huo, Ofisa Masoko wa mradi huo, Alfred Hezron amesema kwa sasa uzalishaji wa mkaa mbadalaa utokanao na makaa ya mawe ni tani 25 kwa mwezi na lengo ni kuongeza uzalishaji hadi kufikia tani 480 kwa mwezi.

Amesema kufanikisha hilo tayari Stamico imeagiza mitambo miwili mikubwa yenye uwezo wa kuzalisha tani 20 kwa saa na kusaidia kuongeza uzalishaji hadi kufikia tani 960 kwa siku na hivo kuwa na uhakika wa mkaa.

Waziri mwenye dhamana ya Mazingira, Dk Suleman Jafo alizitaka taasisi mbalimbali ikiwemo shule, magereza na kambi za jeshi kuunga mkono sera hiyo kwa kuanza kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ili kuokoa raslimali za misitu.

Amesema kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia imefika wakati sasa kwa taasisi hizo kuanza kutumia nishati mbadala yenye athari ndogo katika mazingira husussani mkaa mbadala.

“Tunafurahi kuona Stamico amejielekeza katika utengenezaji wa matumizi ya mkaa mbadala ambao unatokana na makaa ya mawe tumeona sasa changamoto hii ya matumizi ya kuni na mkaa inaondoka,” ameeleza Jafo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles