23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

St. George yamtaka kinda wa Azam

Frid-0cfbaNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

WINGA wa timu ya Azam FC, Kelvin Friday, amewavutia mabingwa wa Ligi Kuu ya Ethiopia, St. George, baada ya klabu hiyo kutuma barua ya kumtaka kinda huyo akafanye majaribio.

St. George kwa sasa inafundishwa na kocha wa zamani wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Mholanzi, Mart Nooij, ambaye amewahi kumuita mara kwa mara Friday kwenye kikosi cha Stars akianzia na Stars Maboresho.

Taarifa iliyotolewa jana katika mtandao wa Azam kupitia kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Saad Kawemba, ilisema tayari wamepokea barua ya mwaliko kutoka kwa mabingwa hao na sasa jambo hilo linashughulikiwa.

“St. George wanamtaka Friday kwa majaribio ya wiki moja na tayari wameshatuma barua rasmi leo (jana) ambayo uongozi umeanza kuifanyia kazi kwani ndio tumeipokea hivyo baadaye tutajua anatakiwa kwenda huko lini baada ya kuwasiliana nao,” alisema.

Winga huyo ni mmoja wa wachezaji waliokulia katika kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji cha Azam na kupandishwa timu kubwa kutokana na uwezo wake wa kupiga mashuti ya mbali.

Endapo Friday atafuzu majaribio yake na pande zote mbili kukubaliana, atakuwa ni mchezaji wa pili kuondoka Azam ndani ya muda mfupi baada ya klabu hiyo kumruhusu winga, Brian Majwega kutua Simba.

Majwega ambaye ni raia wa Uganda aliikimbia Azam na kurudi kwao, lakini aliporejea nchini alianza kufanya mazoezi na Simba huku akiwa na mkataba na timu yake ya zamani jambo lililorahisisha usajili wake.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles