27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

NHIF yazindua kituo

428Na Asifiwe George, Dar es Salaam

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umezindua kituo cha huduma kwa ajili ya kupokea malalamiko kutoka kwa wanachama wao kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa NHIF, Michael Mhando alisema lengo la kuanzisha kituo hicho ni kupunguza kero kwa wanachama wao.

Alisema huduma hiyo itapatikana bure kwa kupiga namba  0800110063 na  kuuliza maswali au msaada  wa haraka kuhusu kadi ya matibabu au huduma katika  kituo  cha matibabu, dawa na vipimo.

Alisema mfumo huo, una uwezo wa kuhudumia wateja 10 kwa wakati mmoja na uwezo wa kutoa majibu moja kwa moja kwa  mlengwa.

Pia wametoa mafunzo kwa watoa huduma  wa  maduka ya dawa yaliyosajiliwa na NHIF namna ya kuwasilisha madai yao kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.

Alisema mafunzo hayo, yametolewa na wahudumu wa maduka ya dawa ya Wilaya ya Kinondoni  na Temeke.

Alisema lengo  la kuanzisha mfumo huo ni kuondoa udanganyifu  na ulaghai  unaofanyika kwa baadhi ya watoa huduma ambao si waaminifu.

“Mfumo huo utaanza rasmi  Januari Mosi mwakani na utasaidia kujua viashiria vinavyoelekea kugushi au kufanya udanganyifu katika huduma zilizotolewa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles