27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Spika awaandikia barua Chenge, Ngeleja

Anne Makinda
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda

NA AGATHA CHARLES
KUTOKANA na kile kilichoonekana kama kugoma kufanya uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge ambazo wenyeviti wao wamehusishwa na fedha za Escrow kwa kutaka kwanza mwongozo wa Spika, Kamati hizo zimeagizwa kufanya uchaguzi huo kabla ya kuanza Mkutano wa Bunge Jumanne wiki ijayo.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, alisema tayari hadi jana Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anne Makinda, alikuwa ameziandikia kamati hizo barua kuzitaka kufanya uchaguzi huo kabla ya Januari 27, Mkutano wa Bunge wa 18 utakapoanza.
“Tayari Spika amewaandikia barua wafanye uchaguzi wa wenyeviti kabla ya Jumanne ya tarehe 27, mwezi huu ili kutekeleza maazimio ya Bunge,” alisema Dk. Kashilillah.
Barua hiyo ya Spika imetoa maelekezo ya kufanyika kwa uchaguzi huo wa wenyeviti wakati ambao tayari kulikuwa na mvutano kuhusu namna ya wenyeviti hao kuwajibika.
Juzi Gazeti la Mtanzania liliripoti mmoja wa Wenyeviti wa Kamati ya Nishati ya Madini, Victor Mwambalaswa kulazimika kuondolewa na maofisa wa Bunge kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi kilichoketi ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.
Danadana hizo za kuwajibika kwa viongozi hao wa Kamati ziliendelea kwa muda tangu Kamati hizo zianze kukutana takribani wiki mbili sasa.
Mbali na Mwambalaswa, mvutano wa kuwajibika ulijitokeza pia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja, wakati kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge akiamua kukaa pembeni mapema tofauti na wenzake.
Chenge, Ngeleja na Mwambalaswa waliamriwa na Bunge kukaa pembeni kutokana na kuhusishwa na kashfa ya fedha za Tegeta Escrow.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles