27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 8, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Soko la Kariakoo laimarisha usafi

AVELINE KITOMARY Na JOHN KIMWERIDAR ES SALAAM

MENEJA wa Afya na Usafi katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam, Donald Sokoni, amewataka wafanyabiashara kuzingatia usafi wa mazingira katika kipindi cha Sikukuu za Krismas na mwaka mpya.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Sokoni alisema mazingira ni masafi hivyo wafanyabiashara hawaruhusiwi kuweka bidhaa zao chini kwani zinaweza kusababisha uchafu.

“Hali ya biashara ni nzuri, kikubwa nawasihi wafanyabiashara waendelee kuimarishausafi wa mazingira ili faida ionekane kwa mkulima na mfanyabiashara,”alisema Sokoni. Meneja huyo pia alisema wafanyabiashara wa soko hilo hawaruhusiwi kuwe kabidhaa chini kwani hiyo haileti tasira nzuri.

Hata hivyo, Sokoni  aliwasihi wafanyabiashara wenye malalamiko na kero mbali kufika ofisini kwake ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.

Mmoja wa wafanyabiashara wa soko hilo, Wiston John alisema hali ya usafi kwa sasa ni nzuri isipokuwa wanayo changamoto ya gharama za mazao kutoka mikoani kuzifikisha Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles