SNEIYA AWATOA HOFU MABINTI

0
1110

NA JANETH MAPUNDA

RAPA anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Bongo Fleva, Husna Deogratius ‘Sneiya’ ame- watoa hofu wasanii wa kike na kuwaomba wasiogope kuonyesha vipaji walivyonavyo.

Akipiga stori na Swaggaz, Sneiya ambaye hivi sasa anatamba na wimbo unaoitwa Nawaza alisema chanzo kikubwa cha Bongo Fleva kuwa na wasanii wachache wa kike ni uoga na hofu ya kukabiliana na changamoto.

“Tusiogope kuonyesha vipaji vyetu hasa sisi wasanii kunao rap kwa sababu muziki wetu hivi sasa una upungufu
mkubwa wa wasanii wa kike,” alisema Sneiya.

Aliongeza kuwa yeye ameamua kufanya muziki wa Hiphop si kwa ajili ya ushindani bali ameamua kufanya hivyo kwa sababu ana uwezo wa kuandika mashahiri pia staili ambazo haijawahi kusikika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here