27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Sitta: Watanzania wakitaka nitakuwa rais

Samuel Sitta
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta

NA RACHEL MRISHO, DODOMA

MWENYEKITI wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, jana ametumia mwamvuli wa Bunge hilo kujipigia debe la urais na kudai kuwa ana sifa za kuliongoza taifa.

Akiwa katika kikao cha 31 cha mjadala wa wazi wa Bunge Maalumu la Katiba mjini hapa, Sitta alisema baadhi ya watu wameanza kumwandama wakidai kuwa kutokana na anavyoliongoza Bunge hilo ameonyesha kuwa hana sifa ya kuwa mgombea urais mwaka 2015.

“Wengine wananikejeli kuwa kwa shughuli hii sifai kuwa rais, mimi sijaomba urais, naifanya kazi hii kama Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, rafiki yangu Juma Duni Haji, kwa hoja zilizo duni kabisa anajaribu kunipima.

“Lakini nasema wanaochagua ni wananchi, inawezekana mwakani wananchi wa Tanzania wakatamani mtu mzima aliyetulia, asiyewaogopa wapuuzi, mtu makini na mwadilifu, basi kama itakuwa hivyo, wajue tu kuna sisi wengine wa kuweza kufikiriwa kwa mambo kama hayo,” alisema Sitta.

Kutokana na hali hiyo, aliwataka wajumbe wa Bunge hilo wasifadhaike na maneno ya kejeli yanayotolewa na watu mbalimbali dhidi yao, yakiwamo yanayohusu posho wanazopokea wakati huu ambapo wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wako nje ya Bunge hilo.

Alisema madai hayo hayawezi kuwa sehemu ya uundwaji wa Katiba mpya ambayo inakiuka sheria zinazoelekeza upatikanaji wake.

Katika maelezo yake, Sitta alikiri kuwa alikuwa anafanya kazi ya kukusanya maoni ya makundi mbalimbali ambayo yaliwasili bungeni hapo wakati kamati za Bunge hilo zikiendelea na majadiliano ya ndani.

“Chombo cha juu cha Tume ya Marekebisho ya Katiba ni Bunge hili, ndiyo maana katika kipindi hiki makundi mbalimbali yametoa maoni na mengine yamekubalika katika kuboresha Katiba,” alisema mwenyekiti huyo ambaye siku zilizopita alikana kuwa alichokuwa akikifanya si kukusanya maoni bali ni kupokea mapendekezo ya kuboresha Katiba mpya.

Alisema yupo imara, na hulka yake juu ya kejeli na matusi dhidi yake, ni kama maji kwenye mgongo wa bata ambaye halowani.

Amshambulia Kubenea

Katika hali isiyo ya kawaida, Sitta alimshambulia mwandishi wa habari, Saed Kubenea na kudai kuwa anatumiwa na wafadhili ili kumchafua.

“Kuna rafiki yangu mmoja anaitwa Said Kubenea, karne za 15-16 hadi 17 wafalme kule Ulaya walikuwa na watu wao wanaitwa ‘Court gesters’, yaani wachekeshaji, wafalme wa Ulaya waliajiri wachekeshaji kwa malengo mawili, moja ni kumsifia mfalme kwa kila kitu, jingine ni kuwasema wale wote ambao mfalme anahisi ni wabaya wake.

“Kwahiyo tuna watu wa namna hii ambao tunaanza kuwaona hata sasa kama Kubenea, ni mchekeshaji wa mfalme tu, kuna mfadhili na wafadhili nyuma yake wanamsogeza… kuna njia nyingi za kupata riziki, tuwasamehe tu waendelee,” alisema.

MTANZANIA ilipotafuta kwa njia ya simu Kubenea ili kuzungumzia tuhuma hizo dhidi yake, hakupatikana hadi tunakwenda mitamboni.

- Advertisement -

Related Articles

3 COMMENTS

  1. Kwa hili la Bunge la Katiba hakika Mheshiwa Sitta umedhihirisha kwamba wewe huheshimu sheria wala, katiba wala mawazo ya wengi. Je hukuona kwamba hatua ya Rais Kikwete kuueleza kinagaubaga umma wa wa Watanzania kwamba kamwe Serikali tatu haziwezi kutokea wakati wa utawala wake tayari alivuruga mchakato na kwamba alikwishakuwekea msimamo wewe ukiwa Mwana-CCM? Kwa nini hukumshauri machakato uanze upya wakati ule ule kuliko kuweka maoni yenu nje ya yale rasmi ya Wananchi? Ple sana Mzee wetu.

  2. Tatizo la waafrika ndio hili. Mtu anafanya makosa, badala ya kujirekebisha anakua mbishi. tume iliteuliwa kwa mujibu wa sheria, bunge lina wabunge ambao ndo wawakilishi wa makundi yooote, sasa iweje mpake kina siwazuri na kalunde nao wende tena kutoa maoni? pole baba lakini hii strategy yako nahisi kama ime backfire.

  3. mh. sita ameonesha dhahiri kabisa kuwa ni mtu asiyejali ushauri na maoni ya wananchi anajali misimamo yake binafsi na misimamo ya chama chake ambayo haifuati misingi ya rasimu ya katiba hata akiwa rais ataongoza nchi kwa kufuata misimamo yake binafsi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles