25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Sita wataka kumrithi Goran Simba

Goran-KopunovicNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM
WAKATI Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic akiendelea kung’ang’ania kuongezewa dau na uongozi wa klabu hiyo, tayari makocha sita wametuma maombi ya kuchukua nafasi yake endapo klabu hiyo itashindwa kufikia dau lake.
Goran bado ameendelea na msimamo wake akitaka kulipwa mshahara wa Sh milioni 28, ambapo uongozi wa Simba umedai kuwa kiasi hicho ni kikubwa na kumtaka hadi kesho awe ametoa jibu kama ataweza kukipunguza.
Habari za uhakika ilizozipata MTANZANIA, zimedai kuwa miongoni mwa makocha hao sita yupo aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Milovan Cirkovic.
“Milovan ameomba kurudi kuendelea kukinoa kikosi hicho sambamba na makocha wengine watano kutoka timu mbalimbali, lakini uongozi haujawajibu chochote hadi sasa,” alisema.
Alisema uongozi umeshindwa kufanya hivyo kutokana na kusubiri maamuzi ya mwisho atakayoyatoa Goran kuhusu dau lake kabla hajaondoka kwenda kwenye mapumziko nchini mwao na kuona kama wataweza kukubaliana.
Alisema wameamua kumpa nafasi hiyo yakujifikiria tena kocha huyo, kutokana na mchango wake mkubwa kwa timu hiyo lakini asipokubali ndipo wataanza kufikiria maombi ya makocha hao.
Goran kwa sasa amekuwa akiwafikirisha viongozi wa timu hiyo ambao walipanga kuendelea naye kwa msimu ujao kutokana na jinsi alivyoweza kuinyoosha timu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles