23.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Khadija Kopa, Diamond kuurudia ‘Nipepee’

Diamond Platnumz feat Khadija Kopa - 'Nasema Nawe'NA THERESIA GASPER
MALKIA wa mipasho nchini Tanzania, Khadija Kopa, anatarajia kufanya ‘remix’ ya wimbo wa ‘Nipepee’ alioshirikiana na mwanaye, Omary Kopa enzi za uhai wake.
Kopa aliweka wazi mpango wake huo wa kushirikiana na msanii, Abdul Nassib ‘Diamond’ hivi karibuni alipotembelea ofisi za New Habari (2006) Ltd zinazochapisha magazeti ya Mtanzania, Rai, The African, Bingwa na Dimba zilizopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Alisema baada ya kushirikiana naye katika wimbo wa ‘Nasema Nawe’ amevutiwa kufanyia kazi wimbo huo kwa kuwa Diamond anavutiwa nao muda mrefu hivyo ameona ni fursa kuufanyia kazi ili kukumbusha mashabiki wao na kumuenzi mtoto wake aliyeimba katika wimbo huo.
“Mimi na Diamond tumepanga kufanya ‘remix’ ya wimbo huo kwa kuwa mimi naujua vizuri naye anaupenda muda mrefu na amekuwa akiuimba mara kwa mara hivyo tunatumaini tutapata kitu kizuri baada ya kukamilisha kuurekodi wimbo huo,’’ alisema Kopa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles