24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

SIRRO: HATUFANYI KAZI KWA TUNGULI

Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro
Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro

Na JOHANES RESPICHIUS – Dar es Salaam

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema halifanyi kazi kwa kwenda kwa waganga wa tiba asili kupiga ‘tunguli’ bali wanapata taarifa kutoka kwa raia wema.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam juzi usiku na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Kamishna Simon Sirro, katika hafla ya kuwaaga askari polisi wastaafu 18 ambao licha ya kuwapongeza, aliwataka kuwa na nidhamu katika jamii na kushirikiana nao pale watakapohitajika.

Alisema kazi ya jeshi ni ngumu na inahitaji ushirikiano wa karibu kati ya wananchi na polisi katika kuhakikisha wanakomesha uhalifu na amani inapatikana nchini.

“Siku nyingine huwa najiuliza je, nitafika siku ya kustaafu nikiwa mzima? Maana kazi ya jeshi ni ngumu, kwa sababu sisi hatufanyi kazi kama vile tunaenda kupiga ‘tunguli’ Bagamoyo, bali tunawakamata wahalifu kupitia taarifa tunazopewa na raia wema,” alisema Sirro.

Pia aliwataka wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mema kwa kuwaepusha kujiingiza katika makundi yasiyofaa.

“Nawataka wazazi na jamii kwa ujumla kuwalea watoto wao katika maadili isije kufika wakati mama au baba ungependa mwanao akuzike, lakini wewe ndiyo unamzika mapema halafu unabaki kulilaumu Jeshi la Polisi,” alisema Sirro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles