30 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Simbachawene awaagiza maofisa elimu kujitathmini

simbachawene

Na MWANDISHI WETU- DODOMA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, amewaagiza maofisa elimu wa mikoa na wilaya kufanya tathmini ya utendaji wao wa kazi ili wabaini upungufu unayojitokeza katika maeneo wanayoyasimamia.

Agizo hilo alilitoa mjini hapa jana baada ya kufanya ziara katika Shule ya Msingi Lufu iliyopo Kijiji cha Lufu, Kata ya Lufu, Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma na alikuta karibu nusu ya wanafunzi wa darasa la tatu hawajui kusoma huku karibu wanafunzi wote hawajui kuandika vizuri.

Aliwataka waratibu wa elimu kata, walimu wa shule za msingi na sekondari kujitathmini katika utendaji wao wa kazi ili kuona kama wana uzalendo kwa utaalamu walionao na kwa mshahara wanaochukua.

Kuhusu alichoshuhudia katika shule hiyo, Simbachawene, alisema wanafunzi hawakuandaliwa vizuri toka darasa la kwanza na walipofika darasa la nne na kufanya mtihani wao hawakufanya vizuri.

“Tafsiri nyingine walimu hawajitumi vizuri na pia mbinu za ufundishaji ili watoto waweze kuandika mwandiko mzuri na zenyewe pengine zinapuuzwa karibu katika shule nyingi hapa nchini.

“Lakini pia inaonekana kitengo cha ukaguzi ubora wa elimu kimekufa hakifanyi kazi yake vizuri na lazima wadau wa elimu nchini wahakikishe kuwa wanalipa uzito unaostahili jambo hilo,” alisema Simbachawene.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles