24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yaipiga bao Yanga Zimbabwe

omary-athuman-mponda*Yamnasa mtoto tishio wa Ndanda

Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

KLABU ya Wekundu wa Msimbazi Simba, ni kama imewapiga bao mahasimu wao Yanga, kwa kufanya mazungumzo na mshambuliaji hatari wa timu ya Ndanda, Omary Athuman Mponda, ili aweze kutua katika timu hiyo kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajia kuanza Desemba 27.

Matajiri wa Simba, Muslei Turwei, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na Msemaji Haji Manara, walitua nchini Zimbabwe, kuweka mazingira ya  kunasa saini ya mshambuliaji huyo ambaye alikuwepo kwenye rada za Yanga ili kuwasaidia katika mzunguko wa pili.

Mponda alikuwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kilichochapwa bao 3-0 na wenyeji Zimbabwe wikiendi iliyopita.

Chanzo cha habari kilichoshuhudia tukio hilo Zimbabwe, kilidai kuwa Mponda ameshafanya mazungumzo na Simba na wanatarajia kumalizana naye wakitua Dar es Salaam, ambapo kikosi cha Stars kilitua jana.

“Simba walivamia Zimbabwe na kufanya mazungumzo, wamebakia kumalizana naye vitu vichache tu atue Msimbazi,” alieleza mpasha habari huyo.

Hata hivyo, dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufunguliwa leo, huku kukiwa na tetesi za nyota mbalimbali kuhama.

Issa Rashid na Ibrahim Ajib tayari wametajwa kuondoka klabu ya Simba na kutua Yanga katika dirisha dogo, kuimarisha kikosi cha Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mbali na wachezaji hao, tetesi zinaeleza kuwa hata Nahodha wa timu hiyo, Jonas Mkude, hana maisha marefu Simba, kwani kocha mkuu mpya wa Yanga, George Lwandamina, ameeleza kutaka kiungo aina ya Mkude hivyo siku za kiungo huyo kuwepo Simba zinahesabika labda Yanga wabadili upepo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles