29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Simba wataka mafanikio ya TP Mzembe

dsc_5479

Na ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

KAMA ulikuwa unafikiri Simba ni timu ya mchezo, basi utakuwa umekosea, kwani hivi sasa Wekundu hao wa Msimbazi hawataki mzaha kabisa, baada ya kubainisha kuwa wanahitaji mafanikio kama ya klabu ya TP Mazembe ya Congo.

Hadi mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu unamalizika, Simba wameweza kumaliza wakiwa nafasi ya kwanza, baada ya kufikisha pointi 35 katika michezo 15, ambapo wamepoteza mechi mbili pekee na hivyo kuwa mbele ya watani zao, Yanga, wenye pointi 32 nafasi ya pili.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili, Meneja wa kikosi hicho, Mussa Hassan ‘Mgosi’, alisema katika usajili wa dirisha dogo, wanahitaji wachezaji wanaojituma na watakaohakikisha Simba inatwaa ubingwa kwa kushirikiana na wale watakaowakuta.

Alisema kocha wao, Joseph Omog, wengi wanamjua kuwa ni muumini wa soka la kisasa linalomtaka kila mchezaji kuwa na maamuzi ya haraka pindi akiwa na mpira miguuni na kwa kuwa kikosi chao tayari kimeshaingia kwenye falsafa hiyo, hata wale watakaobahatika kuongezwa katika dirisha dogo la usajili ni lazima waendane na mfumo huo.

“Hatufanyi usajili kishabiki wala kukomoana, kwetu tutaongeza wachezaji kulingana na matakwa ya benchi la ufundi, lakini lazima hao wanandinga wawe wazuri zaidi ya waliokuwepo kikosini hivi sasa, ili nao wawe wepesi wa kuingia katika falsafa ya Kocha Omog ya soka la kisasa.

“Soka la kisasa linamtaka kila mchezaji kucheza kwa kujiamini na kisha kutumia nafasi atakayoipata vizuri ili kuisaidia timu kupata ushindi, ndiyo maana kocha Omog mara nyingi awape mbinu za kisasa  wanandinga wake kwa kuwa anajua licha ya kuhitaji ubingwa lakini inahitaji mafanikio kama yaliyofikiwa na TP Mazembe,” alisema.

“Kwa hivi sasa mpira wa miguu umebadilika, hivyo lazima Simba iwe na wachezaji wanaojitambua na kujua majukumu yao ndani ya timu, kila mmoja kutumia akili na kufanya maamuzi ya haraka, lakini pia ni lazima wakati wote wawe mchezoni ili ikitokea amepata mpira ajue anaupeleka wapi kwaajili ya kuchangia ushindi wa timu,” alisema.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo MTANZANIA Jumapili linazo, ripoti ya kocha imeitaka Simba iachane na wachezaji saba ambao wameonekana kutokuwa na msaada kwenye mzunguko wa kwanza, lakini pia ikihitaji kusajiliwa kwa wachezaji watatu katika nafasi ya mshambuliaji, beki na kipa atakayesaidiana na Vincent Angban.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles