24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

SIMBA BADO WANAKAZI YA KUFANYA KWA MO

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM


KAMA hauna fedha ni ndoto kufika katika mafanikio.Dunia ya sasa inahitaji fedha kukamilisha kila ndoto unayoota iwe usiku au mchana.

kuna wakati fedha inafanya maisha yawe raini na kukupa faraja lakini pia inaweza kuwa chanzo cha matatizo kabla ya kufika safari ya mafanikio unayotaka.

Kila lengo linahitaji muda kulifikia bila kusahau kuepuka kukata tamaa, juhudi na ushirikiano na watu wengine.

Klabu ya Simba sasa ina fedha itakayowafikisha kwenye ndoto zao na wanachohitaji ni muda tu ili kufika  wanakotaka.

Ukimlisikiliza kwa umakini mshindi  wa zabuni kwenye klabu hiyo Mohamed Dewji ‘MO’  anaonekana kuhitaji u8shirikiano ili kukamilisha ndoto ya klabu hiyo kufika zilipofika klabu kubwa Afrika.

MO anaonesha kudhamilia kuisaidia Simba kuiweka katika ramani ya dunia na kinachobakia ni Simba yenyewe kuwa tayari kuwa eneo hilo.

Kwenye fedha kuna matatizo mengi na muda mwingine ndio huwa chanzo cha vurugu na kutoelewana kwa baadhi ya viongozi na wanachama lakini inawezekana Simba wasifike huko kutokana na katiba na muongozo walioandaa kabla ya kuingia katika mabadiliko hayo ila hakuna anayejua akiwazacho mwingine.

Bilionea huyo ambaye anaimiliki Simba kwa asimilia 50 ya hisa alizonunua za klabu hiyo anamikakati mingi kuelekea msimu ujao na kiu yake kubwa ni kuona Simba ndiyo timu pekee inayotamba na kuzizima timu pinzani za Yanga na Azam ambao zimekuwa zikitoa ushindani kara kadhaa.

Hata hivyo jambo moja kubwa ni kuiombea Simba pamoja na MO wafike kwenye ndoto zao ili kama kufaidika tufaidike wote wapenda maendeleo ya soka.

Kwani sasa hivi Simba inajiandaa na michuano ya kimataifa ambayo mara ya mwisho kushiriki ilikuwa ni mwaka 2012 ilipocheza Klabu Bingwa ya Afrika na kutolewa katika hatua muhimu na Waarabu wa Al Shandy kutoka Sudan.

Timu kama Simba haikupaswa kujifunza sasa kwani viongozi wake wote si wageni katika mfumo wa kiungozi wa soka la Tanzania na baadhi yao ni wale waliofanikisha kuivua ubingwa Zamalek katika Klabu Bingwa Afrika mwaka 2003.

Simba ni timu pekee yenye rekodi nzuri katika michuano ya kimataifa kwani ukiacha kufika fainali ya Caf pia iliwahi kufika fainali za Klabu Bingwa ya Afrika mwaka 1974 ikiwa ni pamoja na kuzifunga timu za Waarabu.

Lakini wakati Simba ikifika fainali ya Caf mwaka 1993, wapo baadhi ya viongozi waliokuwa karibu na timu japo hawakua viongozi wa kuchaguliwa.

Siri ya mafanikio hayo ni ushirikiano  uliokuwa miongoni mwa viongozi, mashabiki na wachezaji hilo pia linaweza kuwa mtaji mkubwa katika kipindi hiki ambacho klabu hiyo inatamani kufanya mambo makubwa zaidi Afrika na kuwa mfano wa kuigwa kwa klabu nyingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles