*Atoa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh milioni 10
*Ni katika kuelekea Sikukuu ya Idd
Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa, (MNEC) Mkoa wa Simiyu, Emmanuel Gungu Silanga, ametoa vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 10 kwa Watu Wenye Mahitaji Maalum, katika Wilaya zote za Mkoa wa Simiyu, pamoja na Magereza yote yaliyopo katika Wilaya tano za Mkoa huo, ili kusherekea vema Sikukuu ya Idd ambayo inatarajiwa kusherekewa wiki
Gungu ametoa vitu hivyo wakati jana akishuhudia Mashindano ya kusoma Quran katika Msikiti Mkuu wa Bakwata, Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, ambapo alisema ametoa vitu hivyo ili kuwezesha Wailsamu wote wa Mkoa wa Simiyu, na watu wenye uhitaji Mkoani humo kusherekea vema Sikukuu ya Idd.
Aidha, Gungu amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kudumisha Umoja na Mshikamano kwa Watanzania, pamoja na kuipongeza Kamati ya Amani ya Mkoa wa Simiyu kwa kumsaidia Mheshimiwa Rais kwa kuhubiri Amani Umoja na Mshikamano, ili kuendelea kuilinda na kudumisha Amani iliyopo nchini.
“Imekuwa kawaida yangu kufurturisha kila Mwaka, lakini kipindi hiki nimekuja tofauti kidogo. Nimeona nitoe kitu kidogo kwa ndugu zangu Waislamu wote wa Mkoa wa Simiyu ilikuweza kusherekea vema Sikukuu ya Idd. Nimetoa Mchele kwa Wilaya zote za Mkoa wa Simiyu, Maharage Mafuta, Tende na Kanga nguo Kanga kwa Wafungwa Wanawake. Pia nimewakumbuka na ndugu zetu waliyopo kwenye Magereza yote ya Mkoa wetu wa Simiyu, watapata vitu kama nilivyovitoa kwa wengine,”alisema Gungu
Gungu ameahidi kushirikina na Waislamu katika kudumisha amani, umoja na mshikamano na kumuunga mkono Mheshimiwa Dk. Rais Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha Mkoa wa Simiyu unakuwa katika nyanja mbalimbali za Maendeleo na Kiuchumi.
Kwa upande wake Shekhe wa Mkoa wa Simiyu, Shekhe Issa Kwezi alimshukuru Mjumbe huyo wa Nec kwa msaada wake huo, ambapo alisema utawawezesha watu wenye uhitaji kusherekea vema sikukuu ya Idd pamoja na Waislamu wote wa Mkoa wa Simiyu.
“Kila mwaka tumekuwa pamoja na Mheshimiwa Mnec Gungu, kwa kweli hujawahi kutuacha kila tunapokuhitaji. Tunakushukuru sana kwa kuwakumbuka Waislamu wa Mkoa wa Simiyu wakati tukiwa tunaelekea kusherekea Sikukuu ya Idd, tunakuombea Dua nyingi Mungu akuzidishie pale ulipotoa,” alisema Shekhe Kwezi.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Faiza Salim akizungumza kwa niamba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Daktari Yahaya Ismail Nawanda aliwapongeza vijana waliyoshiriki katika mashindano hayo ya kusoma Quruan na kuwataka Wazazi na Walezi kuwalea watoto wao katika maadili yaliyo mema.