25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Silaha 228 zasalimishwa kwa jeshi la polisi

Na Ramadhan Hassan,Dodoma 

Serikali imesema jumla ya silaha 228 zimesalimishwa kwa Jeshi la Polisi  huku akiliagiza  Jeshi hilo  kuangalia upya uwezekano wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015.Hayo

Hayo yamebainishwa leo Desemba 6, 2021 jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene na kusema kuwa kufanya hivyo nikuweka utaratibu wa kisheria wa kutengeneza na kuruhusu Magobole kwa kuwa silaha hizo zimekuwa zikitumika kwa shughuli za ulinzi katika jamii.

Waziri Simbachawene amewaambiwa Waandishi wa Habari kuwa hatua hiyo ni katika  utekelezaji wa tangazo la msamaha kwa usalimishaji wa silaha haramu kuanzia Novemba 1 hadi 30, 2021.

“Kwa mchanganuo wa PISTOL 05 sawa na 2.2% ya silaha zote zilizosamilishwa, magobore 174 sawa na 76.3% ya silaha zote zilizosalimishwa, S/gun 38 sawa na 16.7% ya silaha zote zilizosalimishwa, Rifle 10 sawa na 4.4% ya silaha zilizosalimishwa na SMG 01 sawa na 0.4% ya silaha zote zilizosalimishwa.

“Pia imesalimishwa jumla ya mitutu 12 ambapo mitutu 11 imesalimishwa Mkoa wa  Tanga na Mtutu 01 umesalimishwa Mkoa wa Mbeya.

“Kati ya silaha zilizosalimishwa imeonekana kuwa magobore ni asilimia 76.3 jambo linaloonesha kuwa tatizo la utengenezaji wa silaha za kienyeji  yakiwemo magobore ni kubwa hapa nchini,”amesema Sibachawene.

Amesema kufuatia matokeo haya ya usalimishaji wa silaha haramu,Waziri Simbachawene amelielekeza  Jeshi la Polisi kuangalia upya uwezekano wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015 ili kuweka utaratibu wa kisheria wa kutengeneza na kuruhusu Magobole kwa kuwa silaha hizo zimekuwa zikitumika kwa shughuli za Ulinzi katika jamii.

Pia, kufanya misako kwa kutumia taarifa za kiintelelijensia ili kuwabaini na kuwakamata wale wote wanaomiliki silaha kinyume na Sheria na kisha kuwachukulia hatua za kisheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles