22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

SHIRIKA TANESCO LATAKIWA KUANZISHA MADAWATI YA HUDUMA

NA AMON MTEGA,SONGEA


dk-medard-kalemaniNAIBU Waziri wa Nishati na Madini,Dk.Medard Kalemani amelitaka Shirika la Umeme Tanzania  (TANESCO)kufungua madawati ya huduma za umeme,ikiwamo malipo kila kwenye makao makuu ya kata ili kuwaondolea usumbufu kwa wakazi waliyopo mbali na ofisi hizo .

Kalemani alitoa agizo hilo juzi,alipokuwa akizungumza  na wakazi wa Kata ya Liuli Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kwenye mkutano wa hadhara.

Alisema Serikali imejipanga kuhakikisha suala la umeme linawafikia wananchi kwa asilimia 75 ifikapo Mei,2017 hasa kwa kila kijiji kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) .

Alisema ilikufanikisha asilimia hiyo,watu watakaotumia umeme shirika hilo linapaswa kujipanga vizuri ili kuwafikiwa walengwa.

“Nataka  mwende mkawafuate walengwa ambao ndiyo wateja kwenye maeneo yao kwa kufungua madawati ya huduma za kiofisi, kila makao makuu ya kata na siyo kuwasubiri wafiki ofisini kwenu ambazo asilimia kubwa baadhi ya wahitaji wanashindwa kuzifikia kwa wakati,”alisema.

Katika hatua nyingine,aliwaondoa hofu wakazi wa mikoa ya Ruvuma na Njombe ambao wanatumia umeme wa mafuta ambao mara zote umekuwa ukiwasumbua kwa kukosekana kuwa hadi ifikapo mwaka 2017, tatizo hilo litakuwa limekwisha,baada ya kuunganishwa na gridi ya Taifa.

“Nimejionea mwenyewe tatizo la umeme linaloikabili mikoa hii,nimekuja kutegua kitendawili ambacho miaka yote mmekuwa mkiimbiwa wimbo wa umeme wa gridi ya Taifa bila kufikia malengo sasa natamka kuwa hilo limeisha,”alisema

Akiwa mkoani hapa, alitembelea wilaya za Nyasa,Mbinga,Songea Manispaa na mradi mkubwa  unao tarajiwa kuanza kuchimbwa madini aina ya uani uliyopo  katika Mo Muju wilayani Namtumbo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles