27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Shirika la Mikono yetu lazindua kitabu cha Msichana ni Tai

Na Clara Matimo, Mwanza

Wakati Wanawake wote nchini  jana wakiungana na wenzao duniani kote kusherekea siku yao duniani, Shirika lisilo la Serikali la Mikono Yetu limeadhimisha siku hiyo kwa kuzindua kitabu kijulikanacho kwa jina la Msichana ni Tai, Sio Kuu.

Shirika hilo pia limezindua chanel ya Msichana TV pamoja na wimbo wa Msichana ni Tai, vyote vikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wasichana waliokatisha masomo yao kutokana na changamoto mbalimbali hivyo kushindwa kutimiza ndoto zao waweze kufikia malengo yao.

Diwani wa Kata ya Buswelu,  Sarah Ng’hwani, (CCM), akionyesha kitabu cha Msichana ni Tai, Sio Kuku, baada ya kukizindua, kitabu hicho kimechapishwana Shirika lisilola Serikali la Mikono Yetu, linalojishughulisha  kuwawezesha wanawake na wasichana kumiliki rasilimali zalishi ikiwemo ardhi na mifugo ili waweze kujikwamua kiuchumi. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika hilo, Maimuna Kanyamala, Picha na Clara Matimo.

Akizungumza  jijini Mwanza jana wakati wa uzinduzi huo, Meneja Programu wa Shirika la Mikono Yetu, Sophia Nshushi, alisema  kitabu hicho ambacho kinaelezea historia ya baadhi ya malkia waliotawala katika karne ya 16 hadi ya 18 kimelenga kuwahamasisha wasichana waweze kujiamini ili wafikie ndoto zao.

Nshushi alisema uzinduzi huo ni matokeo ya utekelezaji wa mradi ujulikanao kwa jina la  Msichana ni Tai ambao Shirika la Mikono Yetu lilianza kuutekeleza Agosti mwaka jana  hadi mwaka 2023 kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa  Novo Foundation la nchini Marekani katika Kata ya Buswelu iliyopo Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza. 

Afisa Mradi huo, Halima Juma, alisema, lengo lilikuwa ni kuwafikia wasichana 300 waliopo nje ya shule lakini wamewasajili wasichana 305 wenye umri wa miaka tisa hadi 20 ambao walikuwa na ndoto mbalimbali  wakawapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujiamini kupitia simulizi ya Julie Manning ambaye ni jaji  mwanamke wa kwanza Tanzania.

“Mikono Yetu tunajishughulisha kuwawezesha wanawake na wasichana kumiliki rasilimali zalishi ikiwemo ardhi na mifugo ili waweze kujikwamua kiuchumi, kupitia mradi wa Msichana ni Tai, walengwa wamepata mafunzo ya ujasiriamali, afya ya uzazi, haki na wajibu wa msichana pamoja na jinsi ya kujiamini ili waweze kufikia ndoto zao hivyo kuepuka kuwa tegemezi pamoja na  kufanyiwa vitendo vya ukatili.

“Kati ya wanufaika  305, wasichana 12 walikuwa na ndoto ya kuwa waandishi wa habari, tumewapa mafunzo,  leo(jana) tumewazindulia chanel ya Msichana Tv ambayo wameianzisha wenyewe  inapatikana ndani ya Buswelu  Satelite Cable, wanaopenda kuwa wanamuziki  nao tumewawezesha wamerekodi wimbo wao wa Msichana ni Tai,  wengine tunaendelea kuwawezesha ili watimize ndoto zao,”alisema Halima.  

Akizungumza baada ya uzinduzi huo,  mgeni rasmi ambaye ni Diwani wa Kata ya Buswelu,  Sarah Ng’hwani, (CCM), aliahidi kuwatafutia eneo wasichana hao walioko ndani ya mradi ili wajenge kiwanda cha kutengeneza bidhaa mbalimbali kupitia mafunzo  ya ujasiriamali waliyoyapata ikiwemo pampas za watoto.

Mmoja wa wanufaika wa mradi huo,  Asha Ramadhani, alisema  mafunzo aliyopewa na Shirika la Mikono Yetu, yamemsaidia kufikia ndoto yake ya kuwa mwandishi wa habari maana alitamani lakini baada ya kushindwa kuhitimu elimu yake ya sekondari alikata tama na kujiona hana thamani tena katika jamiii lakini  sasa anaona mwanga wenye mafanikio mbele ya maisha yake lengo lake ni kujiendeleza zaidi kimasomo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles