27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

SHILOLE NA UCHEBE WAKO MSITUCHOSHE MASHABIKI

NA SWAGGAZ RIPOTA

PENZI jipya la mwimbaji nyota wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na mshikaji anayejulikana kwa jina la Ashraf Uchebe, wiki hii limetikisa mitandao ya kijamii.

Sababu kubwa ya wawili hao kugonga vichwa vya habari za burudani nchini ni baada ya kuibuka ukurasa mmoja katika mtandao wa Instagram, uliotumia jina la @official_uchebe kuandika maneno yaliyoonyesha mateso anayoyapata kijana, Uchebe katika himaya ya penzi la Shishi Baby.

Jamaa huyo ambaye amedhamiria kuuvunja uhusiano wa Shilole na mapenzi wake pamoja na kumjengea picha mbaya mbele ya jamii alihakikisha anawaamisha mashabiki kuwa hivi sasa wawili hao hawapo tena pamoja.

Na mkasa uliosababisha kuvunjika kwa panezi hilo, huyo jamaa alidai kuwa ni ahadi zisizotimia ambazo Shilole  alimahidi mpenzi wake Uchebe kama kumpa maisha mazuri, kumpa umaarufu na kuhakikisha wanaingia kwenye ndoa jambo ambalo, Shishi Baby akalikanusha kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kuthibitisha kuwa yeye na mpenzi wake (Ustadhi Uchebe) Shilole aliandika maneno haya: Katika maisha hakuna kitu kizuri kama na furaha kuwa na mtu anakupenda na wewe ukampenda bila kuangalia cheo chake au kazi yake kikubwa ni mapenzi ya kweli tu! Nashukuru Mungu nina mwanaume ambaye ananipa elfu kumi kila siku mimi naiona kama milioni wallah cozi inatoka moyoni na kazi yake ya ufundi gereji naithamini @uchebe1.

Shilole pia ameliambia Swaggaz kuwa mpenzi wake, Uchebe ni mgeni wa mitandao ya kijamii. Hatumii Facebook wala Instagram na huyo jamaa anayetumia jina la Uchebe, kuandika mambo yanayoonyesha anamnyanyasa mpenzi wake ana lengo la kuvunja penzi lao.

“Uchebe wa watu ni mgeni wa hayo mambo ya mitandao, ni mtu wa dini sana hata Instagram hatumii hilo jina, kwa hiyo mtu asitumie jina la mchumba wangu kutafuta followers, tupo vizuri na tunaendelea kupendana Mungu akijaalia tunafunga ndoa Desemba 20 mwaka huu” alisema Shilole.

Ngoja niwasanue Shilole na mpenzi wako Uchebe kitu kimoja ambacho huwenda hamkijui kutoka kwa mashabiki wa Bongo Fleva wenye nguvu kubwa huko katika mitandao ya kijamii hasa wanapotaka kumuinua msanii au kumpoteza pale anapozingua.

Mfano mdogo ni ule uliotokea wiki mbili zilizopita ambapo tuliona jinsi mashabiki wengi walivyokuwa upande wa Ali Kiba na kumuacha Diamond Platnumz akiwa na wale mashabiki wake wa damu pekee huku wimbi kubwa la mashabiki  walikuwa upande wa Ally, huo ndiyo ukweli.

Hiyo inaonyesha wazi kuwa mashabiki hawataki kuchoshwa na msanii, hawapendi staa mwenye mashauzi na anayeendekeza zaidi mambo ambayo hayaendani na kazi. Sasa Shilole na mpenzi wako Uchebe endeleeni na mchezo wenu harafu mtaona jamii ikichoka.

Mashabiki wakichoka hizo kiki zenu hawana msamaha, wana wapoteza tu kama walivyo wapandisha kwenye chati. Ndiyo maana huwa nawaelewa sana wasanii ambao huwa hawatangazi wapenzi wao ili shabiki afuatilie zaidi kazi na siyo maisha binafsi.

Hili ni angalizo kwa Shilole, si vyema kutoa nafasi kwa watu kujadili mapenzi yenu kwa sababu utafanya mashabiki wamkariri zaidi mpenzi wako na siyo wimbo wako mpya  wa Kigori, piga kazi mama na mahaba yabaki kuwa yako na laazizi wako, Ashraf Uchebe usiyafanye ya jamii nzima.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles