29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Shibuda akataliwa Tadea

Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda
Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Chama cha Tadea Wilaya ya Nyasa, Joachim Mwingila, amesema hawataki Mbunge wa Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda ajiunge na chama hicho.

Akizungumza Dar es Salaam jana alisema, Shibuda ni mamluki anayetumwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenda kuvivuruga vyama vya upinzani.

“Shibuda ametangaza kwamba, mwakani hataki kugombea ubunge kupitia Chadema baada ya kusema hivyo akadai atagombea kupitia chama kingine.

“Lakini katika mkutano wa Tadea uliofanyika Julai 28 hadi 30, mwaka huu katika Ukumbi wa Salvation Army, Lifa Chipaka alisema yeye kashazeeka kwa hiyo anataka kumwachia chama Shibuda.

“Chipaka na Shibuda wamekubaliana kwamba makao makuu ya chama yatahamishiwa Mwanza kutoka Dar es Salaam. Sisi hilo hatukubaliani nalo na tumeshampa taarifa msajili wa vyama vya siasa kwamba kitendo hicho ni ukiukwaji mkubwa wa katiba ya chama chetu.

“Hatumtaki Shibuda katika chama chetu kwa sababu anatumika na CCM kuangamiza upinzani hapa nchini,” alisema Mwingila.

Alisema wamemwandikia barua Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kumtaarifu kwamba mkutano uliofanywa na Chipaka sio halali.

“Mkutano ule sio halali kwa sababu hata Chipaka mwenyewe sio Rais wa Tadea kwa kuwa aliondoka tangu mwaka 1995,” alisema Mwingila.

Katika hatua nyingine, aliwataka vijana kujiunga na Tadea ili kuimarisha nguvu ya upinzani.

“Nawaomba vijana wajiunge na chama chetu kwa sababu mgogoro uliopo ndani ya chama chetu utakwisha.

“Nashangaa kuona kuna vijana wanang’ang’ania kubaki CCM na wengine wanajiunga CCM ambacho ni chama mufilisi kilichopoteza dira na kilichoshindwa kutatua matatizo ya Watanzania,” alisema Mwingila.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles