23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

‘SHETANI HANA HURUMA’ ANUSURIKA KWENDA JELA

Na KAMILIKE MMBANDO-DODOMA


MTUHUMIWA Boniface Malyango, maarufu kwa jina la Shetani Hana Huruma, amenusurika kifungo kingine cha miaka 32 jela, baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani katika makosa matatu yanayohusiana na ujangili.

Akitoa hukumu hiyo jana, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, Mwajuma Lukindo, alisema Malyango hakutiwa hatiani baada ya mahakama kujiridhisha kuwa hana hatia yoyote.

Pamoja na kunusurika adhabu hiyo, Shetani Hana Huruma anaendelea kutumikia kifungo cha miaka 12 jela alichohukumiwa Machi, mwaka huu, kwa makosa ya uhujumu uchumi na mali zake kutaifishwa.

Wakati Shetani Hana Huruma akinusurika na adhabu hiyo, kaka yake, aitwaye Juma Malyango na wenzake saba, wametiwa hatiani miaka 32 jela kila mmoja, katika makosa matatu yaliyokuwa yakiwakabili.

Makosa hayo ni pamoja na kujihusisha na genge la wahalifu kinyume cha sheria ya hifadhi ya wanyamapori, kukutwa na nyara za Serikali na kosa la tatu ni kukutwa na meno 18 ya tembo,  yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo, adhabu kwa kosa la kwanza kwa mshtakiwa namba moja hadi wa nane ni kwenda jela miaka 10, la pili ni kifungo cha miaka miwili, wakati kosa la tatu washtakiwa wamehukumiwa kwenda jela miaka 20 kila mmoja.

Katika maelezo yake, Jaji Huruma alidai kuwa, wakati kesi ikisikilizwa uliwasilishwa ushahidi wa moja kwa moja ukihusisha bunduki tatu, ambazo zilitumika kama vielelezo na meno 18 ya tembo.

Katika shtaka hilo, washtakiwa hao ni Juma Malyango, Lucas Hosea, Mwinyijamal Igonza, Lucas Mayai, Emmanuel Sindano, Daud Mwaja na Yohana Chamaulaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles