24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Sheria ya mtandao yanasa watano

Suleiman-KovaAsifiwe George na Ester Mnyika, Dar es Salaam

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kutumia vibaya mitandao ya kijamii kufanya uhalifu wa  kutengeneza habari za uongo na uzushi dhidi ya viongozi au watu maarufu.

Akizungumza  na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleimani Kova alisema watu hao wamekuwa wakitumia vibaya majina ya watu maarufu hasa wanasiasa.

Kova alitaja majina ya wanasiasa yanayotumiwa vibaya kuwa ni mgombea ubunge Jimbo la Kibamba, John Mnyika na mgombea urais wa Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na  usalama.

Aliwataja watuhumiwa hao, kuwa ni Joel Lumbay (32), Omar Suleiman wote wakazi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Michael Nickson (32) mkazi wa Tegeta, Patrick Natala  na Maxmillian Msacky wakazi wa jijini Dar es Salaam.

Alisema watu hao, wamekuwa wakituma ujumbe mbalimbali  wakionesha viongozi hao walikuwa wanajadili jambo fulani dhidi ya kundi au chama  kingine cha siasa kwa kutumia mitandao.

“Wana tabia ya kutengeneza ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwa lugha iliyozoeleka kama ‘kuchati,’  lakini mawasiliano hayo hayapo… yanakuwa yametengenezwa ili kutimiza malengo yao. Jambo hili ni kosa la jinai na linaweza kuchochea chuki  katika makundi ya watu,” alisema Kova.

Alisema jeshi hilo linaendelea kuwasaka watu hao kwa kushirikiana  na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

“Kiongozi  au mtu yeyote atakayeona  ameathirika na mbinu  chafu za kihalifu  asisite kutoa taarifa kwa vyombo  vya dola ili hatua za kisheria zichukuliwe mara moja,” alisema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles