25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Nape: CCM itazuia mafuriko kwa kidole

napeNA SARAH MOSSI, LINDI

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema chama hicho kina uwezo wa kuzuia mafuriko hata kwa kidole, achilia mbali mikono.

Nape ambaye ni mgombea ubunge Jimbo la Mtama mkoani Lindi, alisema hayo jana katika mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Nyangao na kuhudhuriwa na mgombea mwenza  wa chama hicho, Samia Suluhu Hassan.

Katika mkutano huo, Nape aliwabeza wanachama waliowania nafasi ya urais kupitia CCM na ubunge, kisha wakatemwa na baadae wakaamua kuhama.

“Mimi sizuii mafuriko kwa mkono, uwezo wangu ni kuzuia mafuriko hata kwa kidole,” alisema Nape.

Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, jimbo lake litaongoza kwa kutoa kura nyingi za urais.“Ni aibu jimbo analotoka katibu mwenezi taifa, lishindwe kutoa kura za kutosha za urais,” alisema.

hatua nyingine, aliitaka Serikali kukirejesha mikononi kiwanda cha kubangua korosho kilichopo ili kiwape ajira vijana wengi ambao hawana ajira jimboni humo.

“Wanatunyonya, wakati mwalimu anaondoka kusini kulikuwa na viwanda vya korosho wakaviua, tunaomba turudishiwe kiwanda chetu cha kubangua korosho vijana wetu hawana kazi,” alisema.

Nape alilalamikia tatizo la maji linalowakabili wananchi wa jimbo hilo na kusema waliowaagusha ni Benki ya Dunia ambayo imeshindwa kutoka fedha za maendeleo kwa wakati.

Akijibu hoja hiyo, Samia alisema mfumo wa stakabadhi ghalani ulianzishwa kwa nia njema na Serikali, lakini watendaji wa vyama vya ushirika waliukoroga.

“Tunataka mkulima wa korosho alipwe fedha zake anapopeleka mazao sokoni na si bonsai…Serikali ya awamu ya tano itaongeza thamani ya bei ya korosho na ufuta, tutajenga viwanda vya ushirika mtakaounda wenyewe ili mpaki vizuri bidhaa zenu,” alisisitiza Samia.

Akizungumzia mfumo wa stakabadhi ghalani alisema Serikali itahakikisha inakarabati mfumo huo na kusisita haitowavumilia watendaji wa vyama vya ushirika wazembe.

Akijibu ombi la Mtama kuwa wilaya, Samia aliwaomba viongozi kufuata utaratibu wa kisheria na kuahidi kulisimamia jambo hilo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles