27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Shamim na mumewe waenda jela maisha kwa biashara haramu ya dawa za kulevya

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaa

Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imewatia hatiani na kuwahukumu kifungo cha maisha jela, Shamim Mwasha na mumewe Abdul Nsembo baada ya kuthibitika kwamba walikuwa wanajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Aidha, mahakama imeamuru dawa hizo gramu 275 za heroin zimeamuliwa ziteketezwe na gari aina ya Discover Landrover litaifishwe na kuwa mali ya Serikali

Hukumu hiyo imesomwa leo asubuhi mbele ya Jaji Elinaza Luvanda baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na pande zote mbili Jamhuri na upande wa utetezi.

Washtakiwa hao walikutwa na kesi ya kujibu mwishoni mwa mwaka jana baada ya mashahidi nane, wa Jamhuri kutoa ushahidi na kuwasilisha vielelezo sita.

Upande wa utetezi unaowakilishwa na Juma Nassoro, Josephat Mabula na Hajra Mungula ulikuwa na mashahidi wateja waona shahidi mmoja.

Shamim na Nsembo wanadaiwa Mei mosi mwaka 2019 walikutwa na dawa za ambapo walikutwa na heroin gramu 275 nyumbani maeneo ya Mbezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles