26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Shaka: Siasa ya ujamaa na kujitegemea haijakufa

MWANDISHI WETU-MOROGORO



KATIBU wa CCM Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamdu Shaka, ameibuka na kusema kuwa chama hicho kinatekeleza siasa ya ujamaa na kujitegemea kwa vitendo.

Amesema hatua ya Serikali kuamua kusomesha watoto bure elimu ya msingi na sekondari na kutatua changamoto ya madawati kwa wakati, ni moja ya misingi ya siasa za ujamaa na kujigemea.

Shaka ambaye aliwahi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mahafali ya kwanza ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari Open.

Alisema anayefikiria siasa ya ujamaa na kujitegemea imekufa basi atakuwa haijielewi.

“Serikali inaposomesha wanafunzi bure, kutafuta madawati, kulipa mishahara walimu, kujenga vyuo vikuu, kutafuta vifaa vya kufundishia, vitabu vya ziada na kiada, zahanati na hospitali, ni utekelezaji chini ya siasa ya ujamaa.

Alisema Watanzania hawana shauku wala ndoto ya kutaka mabadiliko ya utawala kwa kutegemea wenye mawazo duni waliokosa dira na malengo, huku Serikali ya CCM ikijibadili kimfumo na kisera kukidhi matakwa ya wakati katika sekta ya elimu.

“Ili kufikia malengo ya mafanikio, Serikali ni lazima iwe na muundo, mpangilio wa kisera, mfumo wa kioganaizesheni, uhamasishaji na mipango ya kukuza elimu ya msingi, sekondari na elimu ya juu na inabopidi hujibadili kulingana na matakwa ya wakati,” alisema Shaka.

Alitoa pongezi kwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sanyansi na Teknolojia kwa kufanya mabadiliko ya kimfumo na kisera ili kukidhi mahitaji ya nyakati kwa kutengeneza wahitimu watakaokimbizana na mazingira ya kiuchumi na kisiasa kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya uchaguzi 2015/2020.

Alisema juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika kuimarisha sekta ya elimu ni kubwa ikiwa ni pamoja na kuongeza bajeti ya wizara, mchango wa sekta binafsi katika kudahili wanafunzi wa vyuo vya ufundi, mafunzo na elimu ya ufundi sambamba na kusimamia sera ya elimu na mafunzo ya ufundi kama ilivyoelekezwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles